Posts

Showing posts from 2014

wafahamu wasanii wa Nigeria

Image
This list includes all music genres e.g. Rnb, pop, Rap / HipHop, Rock, Reggae, Naija, Blues, Jazz, Highlife and Gospel Singers. A-Z List below; A Ada Alabai Amaray Asa Ayinla Omowura Ay.com B Baba Fryo Banky W Black Magic Bobby Benson Boogey Bongus Ikwue Bouqui Bracket Brymo Bright Chimezie Buchi Burna Boy C Capital FEMI Celestine Ukwu Chamillionaire Chiddy Bang Chidimma Chinyere Udoma Chris Mba Choco Girl Cidyrella Cyrus Da Virus D Dagrin Dammy Krane Darey Art Darey Un Darey.ted Dayo Bello Davido D'banj DJ Zeez Dizzy Don Jazzy D’Prince Dr Sid Dr. Victor Olaiya Duncan Mighty Durella E Ebenezer Obey Edu Ghana Eedris Abdulkareem ELDee Emma Nyra Emeka Morocco Maduka Erigga New Money Evangelist Bola Are Eric Obuh Esther Igbekele Eva Evi-Edna Ogoli F Faze Fela Kuti Femi Kuti Fatai Rolling Dollar Funmi Williams Flavour N’abani G Goldie Gozie Okeke GM Compere GT da guitarman H H-man Harrysong He...

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z

Image
This list includes all music genres e.g. Rnb, pop, Rap / HipHop, Rock, Reggae, Naija, Blues, Jazz, Highlife and Gospel Singers. A-Z List below; A Ada Alabai Amaray Asa Ayinla Omowura Ay . com B Baba Fryo Banky W Black Magic Bobby Benson Boogey Bongus Ikwue Bouqui Bracket Brymo Bright Chimezie Buchi Burna Boy C Capital FEMI Celestine Ukwu Chamillionaire Chiddy Bang Chidimma Chinyere Udoma Chris Mba Choco Girl Cidyrella Cyrus Da Virus D Dagrin Dammy Krane Darey Art Darey Un Darey.ted Dayo Bello Davido D'banj DJ Zeez Dizzy Don Jazzy D’Prince Dr Sid Dr. Victor Olaiya Duncan Mighty Durella E Ebenezer Obey Edu Ghana Eedris Abdulkareem ELDee Emma Nyra Emeka Morocco Maduka Erigga New Money Evangelist Bola Are Eric Obuh Esther Igbekele Eva Evi-Edna Ogoli F Faze Fela Kuti Femi Kuti Fatai Rolling Dollar Funmi Williams Flavour N’abani G Goldie Gozie Okeke GM Compere GT da guitarman H H-man Harrysong Henrisoul I Ibiso Ice Prince Iceberg Slim I.K Dairo Ikenga Superstars ill Bliss i-Mik...

Andre 3000 Is Turning His OutKast Jumpsuits Into T-Shirts

Image
It might be awhile until we hear new music from Andre 3000 but the OutKast co-founder and style risk-taker knows how to ease the wait. Andre has been spending his free time gearing up for the release of a new t-shirt line inspired by those thought-provoking jumpsuits he wore throughout OutKast’s reunion tour that are currently hanging in a museum in Miami. Cue “ So Fresh, So Clean .” Getty Images It was actually fans who inspired the idea. “People have been asking me where can I get that shirt that says ‘I love big girls,’” the rapper explained to Hard Knock TV . Among the other slogans he wore: “children of the cornbread,” “have you stopped growing?,” “make love not war,” “teacher’s deserve more,” “across cultures, darker people suffer most. why?”​ Even though the jumpsuits were designed by Linda Stokes, 3 Stacks came up with the idea. “It really started off as one message and I continued it from there. They are thoughts I am having, and I’m having fun w...
Image
  Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amewataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaounda kamati hiyo, kufanya kazi kama ilivyo kamati yake kwa Tanzania Bara. Zitto aliyasema hayo jana kwenye semina ya wawakilishi hao iliyofanyika jijini hapa ambapo alisema, kamati husimamia matumizi yote ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoidhinishwa na baraza na kutoa taarifa zake kwa Umma. Alisema hesabu za Serikali huendana na Ripoti ya CAG ambayo ndiyo nyenzo kuu ya Baraza katika kusimamia fedha za umma. Hata hivyo, Zitto alisema PAC inapoona inafaa, huagiza ukaguzi maalumu kwenye maeneo mahususi na njia hiyo imesaidia kuibuliwa kwa mambo mengi ya ufisadi wa fedha za umma kwa Tanzania Bara. “Kuna nyakati mkaguzi anakuwa haoni masuala fulani hadi anapoombwa na vyombo vingine na hata wananchi…Ni vyema Kamati ya PAC Zanzibar kutumia pia njia hii ili kuimarisha usimamizi bora wa fedha za umma kwa Zanzibar kama ilivyo sasa katik...

Watumishi waliotajwa kashfa ya escrow wako kazini

Image
Dar es Salaam. Watumishi wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), waliotajwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow wanaendelea na kazi wakisubiri taratibu za utumishi wa umma kabla ya kuchukuliwa hatua. Akizungumza na mwandishi wetu kuhusu hatua zilizochukuliwa baada ya agizo la Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kutaka wafukuzwe, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo alisema jana kwamba hawajachukuliwa hatua hadi taarifa za uchunguzi za vyombo vya dola itakapotolewa. Watumishi wawili, mmoja alitajwa katika taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kutokana na matokeo ya ukaguzi maalumu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu kashfa hiyo kwamba aliingiziwa Sh1.6 bilioni bila maelezo. Mwingine katika kashfa hiyo, badala ya kuandika Dola za Marekani 6 milioni aliandika Sh6 milioni na badala ya kuandika Dola za Marekani 20 milioni, aliandika Sh20 milioni. Kutokana na taarifa hizo wakati wa mkutan...

baiskeli ya dhahabu yazinduliwa Uingereza, bei yake ni sh.milion 676.5

Image
NI rahisi sana kwa watu kulalamikia gharama ya kununua baisekli wengi wakitaka bei nafuu. Baiskeli nyingi nchini Uingereza huuzwa kwa pauni 1,000 sawa na shilingi milioni 2.7 za Tanzania ambazo kwa watu wengi nchini humo ni fedha nyingi sana. Hata hivyo baiskeli mpya iliyotengezwa kwa dhahabu imezinduliwa nchini humo. Bei yake? Pauni 250,000 sawa na milioni 676.5 za Tanzania. Bei hii ni ghali hata kuliko bei ya gari jipya aina ya Ferari. Baiskeli hiyo imetengenezwa na kampuni ambayo hutengeza vitu vya kifahari, Goldgenie na imetengezwa kwa dhahabu. Kiwango cha dhahabu iliyotumiwa ni karati 24. Wataalamu wa kampuni hiyo ya Goldgenie, wameweka dhahabu katika vyuma vya baiskeli hiyo vyote ikiwemo mnyororo na mfumo unaofanya baiskeli kwenda na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu. Mkurugenzi wa kampuni iliyotengeza baiskeli hii anasema inaweza kuendeshwa katika barabara kama baiskeli nyinginezo. Source: BBC

Hii ndio sababu ya Diddy kumpiga Drake

Image
Tmz imeripoti kuwa wimbo uliomfanya Drake apigwe na Puff Daddy ni “0 to 100/ The Catch Up” ambao mpaka sasa umetajwa kuwania tuzo mbili za Grammy kama Best Rap Performance na Best Rap Song. Diddy aligombana na Drake jumatatu asubuhi baada ya sherehe ya siku ya kuzaliwa na Dj Khaled nje ya club ya LIV huko Miami Beach na sababu ikiwa Diddy alihisi amekosewa heshima na Drake. Producer maarufu Boi-1da aliwapa Diddy na Drake wimbo huu ili warekodi miezi nane iliyopita ila Drake alikwenda kurekodi wimbo huu mwenyewe bila kumwambia Pdd kitu ambacho kilimkasirisha Pdd. Diddy alimuona Drake nje ya Club LIV nakuamua kuzungumza naye ndipo Drake alionyesha madharau, kabla hajampiga Pdd alimwambia “Hutokaa kunikosea heshima tena” “You’ll never disrespect me again” .

Kilio cha Albino Tanzania

Image
Mtobi Namigambo, ni mvuvi anayeuza samaki, amekaa kwa utulivi nje ya nyumba yake ya matope katika kisiwa cha ukerewa mahali ambapo zamani palikuwa makao ya albino lakini kwa sasa si hivyo. Mtoto wake wa miaka nne May Mosi ameketi kwenye paja lake akionyesha umarufu wake wa hisabati kwa kuhesabau moja hadi kumi kwa ujasiri. Mara kwa mara Mtobi anamtazama mke wake, Sabina, ambaye ameketi kwa mkeka kando yake akitayarisha chakula cha jioni. Watoto wake wengine wawili wanachezea hapa karibu na pia wamejaliwa na mtoto mchanga amabye yuko chumbani analala. May alipokuwa na umri wa miezi mitatu, aliponea jaribio la kutekwa nyara.   Albino wanauawa kinyama kwa ajili ya imani potovu  " nilikuwa nimeenda ziwani kuvua samaki. walikuwa pekee yao nyumbani wavamizi walipokuja, mke wangu alitorokea kwa dirisha na kukimbillia usalama akiwa na May, na akawawacha watoto hawa wawili nyumabani ambao hawakuwadhuru kabisa", Mtobi ananiarifu. "Wavamazi hao walikuwa wakimtak...

Muhubiri awabaka wanawake akidai kuwaponya

Image
  Muhubiri wa zamani aliyedai kuwa na 'nguvu za kuponya' amepewa adhabu ya kifungo cha nje cha miaka ishiriki kwa kumyanyasa kimapenzi mwanamke mmoja nchini Australia. Muhubiri huyo alidai kutumia kile alichokiita 'nguvu za kipekee' za uponyaji kumdhalilisha kimapenzi mwanamke huyo akisema kuwa alikuwa na mashetani katika sehemu yake ya siri. Omar Sheriff, mwenye umri wa miaka 67, alimwambia mwanamke huyo mnamo mwaka 1994 kwamba alikuwa na mashetani mwilini mwake na kwamba mashetani hayo yalipaswa kuondolewa kwa njia maalum katika kiwanda chake cha fanicha mtaani Campbellfield. Kwa mujibu wa taarifa za jarida la 'The Age', jaji Jane Patrick alifahamishwa kuwa Omar alidai alikuwa na nguvu kubwa sana za kimiujiza na alimuonya mwanamke huyo aliyekuwa na miaka 30 kwamba angefariki ikiwa mashtenai hayo hayangetolewa kutoka katika sehemu yake ya siri. Alisema alikuwa na utabiri kuhusu maisha yake na kumwambia kuwa angepata shida kubwa sana ikiwa asi...

Mwanawe Rais Zuma hatiani Afrika Kusini

Image
  Jopokazi moja nchini Afrika Kusini limesema kua mwanawe Jacob Zuma hakua makini alipokuwa anaendesha gari hadi kusababisha ajali ya barabarani ambapo mwanamke mmoja alifariki. Awali kiongozi wa mashitaka hakuwa tayari kumchukulia hatua zozote za kisheria mwanawe Zuma. Sasa atakabiliwa na shinikizo za kumfungulia mashitaka. Gari la Duduzane Zuma aina ya Porsche iligonga gari dogo la abiria mjini Johannesburg mwezi Februari, na kumuua mwanamke huyo papo hapo. Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani mjini Johannesburg anasema uamuzi huo unaonyesha uhuru wa vyombo vya sheria nchini humo. Katika nchi ambapo swala la usawa bado ni tete, mahakama ndio mojawpao ya sehemu chache ambapo usawa unapatikana kwa wananchi na mwanawe Rais hajasazwa kwa hilo. Rais Zuma ana watoto 21 na ameoa mara sita. Duduzane mwenye umri wa miaka 30 aliambia jopokazi hilo kwa alipoteza mwelekeo wa barabaraalipokuwa anaendesha gari na kuingia ndani ya maji taka. Hata hivyo hakimu alimwambia kwamba h...

Ebola bado tishio Sierra Leone

Image
  Maafisa wa Afya nchini Sierra Leone wamegundua miili kadhaa katika maeneo ya mgodi wa Almasi, na kusababisha hofu kuwa pengine ugonjwa wa Ebola haujaripotiwa ipasavyo. Shirika la afya duniani,WHO limesema limebaini kisa hiki kipya mashariki mwa mji wa Kono, timu ya Wataalamu imepelekwa Kono kufanya uchunguzi kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Ebola. Watu 6,346 wamepoteza maish akutokana na ugonjwa huo na zaidi ya 17,800 wameathirika na Ebola. Sierra Leone ina idadi kubwa zaidi ya Watu wenye Ebola Afrika Magharibi, ikiwa na Watu walioathirika 7,897 tangu kuanza kwa ugonjwa huo. WHO imesema katika kipindi cha takriban siku 11 mjini Kono, Miili 87 ilizikwa. Miili ya Watu waliokufa kutokana na maradhi ya Ebola ni hatari kwa maambukizi hivyo huzikwa kwa uangalifu mkubwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

angalia picha za yule housegirl aliyemtesa mtoto akiwa mahhakamani leo

Image
Kwa mara ya pili yule msichana anayetuhumiwa kwa kesi ya kumpiga mtoto Uganda amepandishwa Mahakamani jana December 10, tarehe ambayo Mahakama ya Uganda ilipanga kutoa hukumu ya msichana huyo. Msichana huyo  Jolly Tumuhirwe , alipandishwa Mahakamani siku ya Jumatatu wiki hii ambapo alikiri kutenda kosa hilo na kuomba msamaha, amerudishwa tena gerezani mpaka December 16, siku ya Jumanne ambapo atapandishwa tena Mahakamani kwa ajili kesi yake kuendelea kusikilizwa.. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Buganda Road Jumanne ya wiki ijayo.

mwana FA na AliKiba wakishoot video ya kiboko changu

Image
Sina Shaka na wewe mtu wa nguvu utakuwa umeshaisikiliza single mpya ya Hamisi Mwinjuma aka Mwana FA ‘Kiboko Yangu’ aliyomshirikisha Ali Kiba ambayo inaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio. Good news ninayotaka kukupatia ni kwamba wakati single hiyo ikiendelea kufanya vizuri kwenye spika za radio yako soon inatarajiwa kuona kwenye chati za TV na hizi ndio baadhi ya picha za Behind  The Scene ambazo zikimuonesha Mwana FA na Ali Kiba wakiwa location katika uandaaji wa video hiyo mpya Kiboko Yangu. . . . Ali Kiba na Mwana FA wakiwa Location katika utengenezaji wa video mpya hiyo Kiboko Yangu. Ali Kiba akiwa na Warembo katika utengenezaji wa video hiyo mpya. chanzo www.millardayo.com

ziwa nyasa bado ni utata kati ya Malawi na Tanzania

Baada ya kutokea vuta nikuvute kati ya nchi hizo mbili zilizokuwa marafiki wa miaka mingi, marais wastaafu kutoka Msumbiji, Joaquim Chissano, Festus Mogae wa Bostwana na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini walipewa jukumu la kutafuta maridhiano. Kile kilichoonekana kuanza kama mzaha kati ya Tanzania na Malawi kuhusu umiliki wa Ziwa Nyasa, sasa kimeanza kuchukua sura mpya kwa kila nchi kuendelea kutekeleza kitu inachokiamini kuwa ni sahihi. Baada ya kutokea vuta nikuvute kati ya nchi hizo mbili zilizokuwa marafiki wa miaka mingi, marais wastaafu kutoka Msumbiji, Joaquim Chissano, Festus Mogae wa Bostwana na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini walipewa jukumu la kutafuta maridhiano. Hivi karibuni marais hao walikutana na Rais Peter Mutharika kwa ajili ya kuzungumzia jambo hilo, lakini kwa bahati mbaya walichodhani kuwa ni jambo dogo, kiligeuka kuwa ‘mfupa mgumu’ baada ya rais huyo kusema Tanzania haimiliki hata inchi moja ya Ziwa Nyasa. Kama hiyo hai...

Bibi harusi wa miaka 14 amuua mumewe kwa kupinga kuolewa

Bi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za harusi yake. Kesi hiyo imewashangaza wanaharakati wa haki za kibinaadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume anayemzidi umri zaidi ya mara mbili yake anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala siyo muhalifu Msichana huyo aliyetambulika kwa jina la Wasila Tasiu kutoka familia maskini katika eneo lenye idadi kubwa ya Waislamu huenda akakabaliwa na adhabu ya kifo Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana wa miaka 7 anayejulikana kama Hamziyya ambaye alikuwa akiishi katika nyumba moja na Tasi’u pamoja na mumewe Umar Sani wakati bi harusi huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho. Akizungumzia zaidi kuhusu kisa hicho ambacho kimevuta hisia za wengi msichana huyo wa miaka 7 alisema kwamba Tasi’u alimpa fedha ili kununua sumu ya panya kutoka d...

sakata la Escrow Wabunge waungana

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana lilikuwa moja dhidi ya utoaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), huku baadhi ya mawaziri wakitofautiana na taarifa ya Serikali ya utetezi wa suala hilo. Kabla ya kuungana huko kwa wabunge, Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha za Serikali (PAC), Kabwe Zitto alihitimisha hoja ya kamati hiyo na Bunge kuingia katika hatua ya kufanya uamuzi wa maazimio ya Bunge dhidi ya watuhumiwa wa uchukuaji wa fedha hizo. Awali kabla ya kufikia hatua ya maazimio, ambayo iliendelea mpaka jana usiku, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alikiri kuwa katika fedha zilizochotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuna kodi ya Serikali na aliagiza wote walionufaika na fedha hizo kulipia kodi ifikapo Desemba 31, mwaka huu. Alisema Serikali ilipaswa kulipwa Sh bilioni 26.97, lakini hadi sasa imelipwa Sh bilioni 4.21. Akichangia mjadala kuhusu taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bun...

Waliokufa na Ebola watimia 7,000

Takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO, zinaonesha kuwa watu karibu 7,000 wamefariki hadi sasa kutokana na Ebola, karibu wote Afrika Magharibi. Hao ni watu zaidi ya elfu moja kuliko idadi iliyotangazwa na WHO Jumatano tu. Vifo vingi zaidi vimesajiliwa Liberia. WHO inasema watu zaidi ya 16,000 wameugua Ebola hadi sasa. Waandishi wa habari wanasema kuongezeka kwa idadi ya waliokufa siyo lazima inamaanisha ugonjwa unazidi kutapakaa kwa kasi kwa sababu takwimu nyengine ni za zamani. Na Rais Francois Hollande wa Ufaransa amezuru Guinea, kiongozi wa kwanza asiyekuwa Muafrika kuzuru moja kati ya nchi tatu za Afrika Magharibi zilizoathirika sana na Ebola. Bwana Hollande alisema alitaka kuleta ujumbe wa matumaini kwa watu wa Guinea: "Ufaransa inaweka mfano - tumefanya hivyo kifedha kwa kutoa dola 125 milioni. Lakini mbali ya msaada wa mali, utu ndio muhimu zaidi. Na Guinea inapochukua hatua za kuuguza na kuzuwia Ebola isisambae, hivyo inasaidia uli...

rais kikwete apona saratani

Image
  Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema amepona saratani baada ya kufanyiwa upasuaji mapema mwezi huu nchini Marekani. Kiongozi huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 64 ametoa hotuba kwa taifa kuelezea afya yake.. "Niligundulika kuwa na hatua ya pili ya saratani ya kibofu, ambayo baadaye ikaonekana kuwa ni hatua ya kwanza," alisema Kikwete katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kupitia televisheni akiwa uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam baada ya kurejea kutoka Marekani. Aliongeza kuwa madaktari wamesema sasa hali yake shwari: "Madaktari walisema saratani haikuenea katika sehemu nyingine za mwili na baada ya upasuaji sasa wamesema nimepona saratani." Alisema aligundulika kuwa na saratani ya kibofu zaid ya mwaka mmoja uliopita na alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins Hospital tarehe nane Novemba. Kikwete ambaye anamaliza muhula wake wa pili mwakani amesema wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao ili wagund...

Ukawa wamtia kitanzi Sitta

Image
UAMUZI uliofikiwa na viongozi wa vyama vya siasa na Rais Jakaya Kikwete umemweka katika wakati mgumu Mwenyeki wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta kuahirisha au la vikao vya Bunge hilo. Hii inafuatia Rais Kikwete na viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kukubaliana kusitisha Bunge la Katiba Oktoba 4 tofauti na ratiba ya Sitta ambayo inaonyesha vikao vitaendelea hadi Oktoba 31 atakapomkabidhi rais katiba iliyopendekezwa. Vilevile kwa tafsiri ya uamuzi huo, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) watakuwa wameibuka kidedea kwani tangu mwanzo walikuwa wanataka Bunge hilo liahirishwe hadi maridhiano yapatikane. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo, alisema katika makubaliano ya kikao chao na rais kilichofanyika juzi Ikulu ndogo mjini hapa, walikubaliana kwa pamoja kuwa Bunge la Katiba liendelee hadi Oktoba 4. Kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa imetolewa mara baada ya awamu ya pili ya Bunge la Katiba kuanza Oktoba 10 hadi 21, ndiyo waju...

Dk. Slaa asema hana barua ya msajili

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema hajawahi kupokea barua yoyote kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, inayowataka waitishe mkutano wa Kamati Kuu ili kufanya marekebisho ya Katiba yao. Wakati Dk. Slaa anatoa kauli hiyo, Julai, mwaka huu, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa chama hicho, John Mnyika, alizungumza na vyombo vya habari kuwa Agosti, 2006 walifanya marekebisho makubwa ya Katiba ikiwamo kifungu kilichokuwa kinaweka ukomo wa uongozi. Juzi, Jaji Mutungi akizungumza na gazeti hili, alieleza kuwa kinachotokea sasa ndani ya chama hicho ni matokeo ya kupuuzwa ushauri wake wa kukitaka kifanye marekebisho ya Katiba yake. Kauli za viongozi hao zilitokana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwekewa pingamizi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Tabora, Kansa Mbarouk, ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya uenyekiti taifa, akidai chama chake kimekiuka Katiba na maagizo ya msajili. Barua ya Msajili wa Vyama ...

WAZIRI WA AFYA NA NAIBU WAKE WATEMBELEA HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA, ZANZIBAR

Image
Waziri wa Afya Mh. Rashid Seif akiongozana na Naibu wake Mh. Mahmoud Thabit Kombo wakitembelea eneo la Hospitali ya Mnzammoja katika ziara yake ya kutembelea Hospitali hiyo. Mkuu wa kitengo cha maradhi ya kisukari katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja Dkt Miskia Ali akitowa maelezo kwa Waziri wa Afya juu ya kadhia ya maradhi hayo. Waziri wa Afya akipata maelezo ya shughuli za Maabara kutoka kwa mtaalamu wa Maabara wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Marijani.

Mtoto wa Obasanjo apigwa risasi Nigeria

Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olesugun Obasanjo amejeruhiwa kwa risasi wakati wa mapambano na wanamgambo wa kiislamu Boko Haram. Luteni Kanali Adeboye Obasanjo alijeruhiwa siku ya jumatatu wakati jeshi la Nigeria lilipokuwa likipambana kuudhibiti mji wa Michika karibu na mji wa Mubi mji uliokuwa ukidhibitiwa na wanamgambo katika jimbo la Adamawa. Msemaji wa zamani wa Olusegun Obasanjo ameiambia BBC kuwa kanali Adeboye anaendela vizuri. Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao, wanajeshi wameondoka kwenye kambi za kijeshi na chuo katika jimbo hilo kufungwa. Wanamgambo wa Boko haram wamedhibiti miji mingi kaskazini mashariki na kutangaza kuwa himaya za kiislamu

Mlipuko waua viongozi wa waasi Syria

Wanachama 50 wa kundi moja la waasi wa Syria wameuawa au kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga. Vyombo vya habari vya serikali na wanaharakati wanasema mshambuliaji wa kujilipua aliilenga nyumba moja katika jimbo la Idlib, ambamo viongozi wa Ahrar al-Sham walikuwa wakikutana. Kamanda wa kikundi hicho Hassan Abboud ni miongoni mwa watu waliouawa. Kiongozi huyo ameuawa pamoja na makamanda wengine wa ngazi za juu wa kikundi hicho. Shambulio hilo limefanywa na mtu aliyejilipua katika mji wa Ram Hamdan kaskazini magharibi mwa Syria. Ahrar al Sham ni sehemu ya kikundi cha Islamic State, muungano wa vikundi saba vya waasi wa kiislamu nchini Syria.

Jack Patrick apewa hukumu ndogo China

Image
BAADA ya kushikiliwa kwa takriban miezi tisa kwa kesi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye Video Queen maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela huku kukiwa na uwezekano wa kupunguziwa adhabu ikawa ndogo zaidi, Amani linaibumburua habari kamili. HUKUMU NYEPESI? Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Jack, modo huyo alihukumiwa Jumatatu iliyopita (Agosti 11, mwaka huu) kwenye Mahakama ya Macau huko Hong Kong ambapo hukumu hiyo ilitofautiana na adhabu nyingine za madawa nchini humo ambazo huwa hukumu yake ni kunyongwa hivyo ya Jack kuonekana nyepesiii! KWA NINI NYEPESI? Kikimwaga data, chanzo hicho makini kilidai kwamba, hukumu hiyo ya Jack ni nyepesi ukilinganisha na hukumu nyingine za madawa ya kulevya zinazotolewa nchini China ambapo hakimu alitumia muda wa dakika 27 tu kuisoma. “Hukumu za madawa ya kulevya zinatofautiana nchini China. Kuna baadhi ya majimbo kama Beijing huwa wao ikithibitika umebeba madawa ya kulevya, una...

Wood ajiondoa katika kombe la Ryder

Image
Tiger Wood ajiondoa mashindano ya kombe la Ryder Mchezaji nyota wa gofu Tiger Wood wa Marekani, amejiondoa katika mashindano ya kombe la Ryder baada ya kushauriwa na madaktari wake. Tiger amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo mara kadhaa na kufikia usiku wa kuamkia hii leo ameamua kutangaza kujitoa kwenye michuano hiyo ya kimataifa. Tiger amemuomba kocha wa timu ya Taifa ya Marekani Tom Watson amuwie radhi kwani wataalamu wake wa Afya wamemtaka apumzishe mgongo wake wenye matatizo na hata wamemzuia asifanye mazoezi yeyote.

fasheni zilizopo sokoni

kliniki ya kusaidia watu kujiua

Takribani waingereza 800 ambao wamechoka maisha waliyo nayo kutokana na kusumbuliwa na magonjwa mbali mbali wamejiunga kwenye foleni ya kusubiria kifo katika kliniki ya Diginitas ya nchini Uswizi. Taarifa za magazeti ya Uingereza zilisema kwamba waingereza 800 ambao wanasumbuliwa na magonjwa mbali mbali ambayo hayana tiba ambao wanataka wafariki muda wowote baada ya kuchoka maisha waliyonayo wamejiorodhesha kwenye foleni ya kusaidiwa kujiua kwenye kliniki ya Diginitas iliyopo nchini Uswizi. Uswizi ndio nchi pekee ya ulaya ambayo inaruhusu watu kusaidiwa kujiua pale wanapoona magonjwa yao ambayo hayana tiba yanawatesa kwa muda mrefu. Kliniki ya Diginitas huwasaidia watu wanaotaka kujiua kwa kuwapa dozi kubwa za madawa ambazo husimamisha mapigo yao ya moyo na kuwaua taratibu wakiwa wamelala. Watu wengi ambao hujiua kwenye kliniki hiyo ni wale ambao wanasumbuliwa na magonjwa yasiyotibika kama vile kansa na mengineyo ambayo huwa yamefikia hatua za mwisho mwisho. Ni kosa la jinai kumsaidia ...

treni la Uswiswi lapata ajali

Image
Treni lililobeba abiria zaidi ya 200 limepata ajali kwa kutereza pembeni ya reli na kusababisha baadhi ya mabehewa kuwa nje ya reli. Abiria waliokuwemo ndani ya treni hilo walilazimika kukimbilia upande wa pili wa treni hilo ili kuepuka lisidondoke kwenye maporomoko.  Juhudi hizo zilisaidia na hakuna mtu aliyefariki kwenye hiyo ajali lakini watu 11 walipata majeraha na watano kati yao kupata majeraha makubwa. Ajali hii imetokea kwenye mlima ya nchini Uswisi toa maoni yako

mashindano ya karate ya dunia kufanyika Tanzania

Image
Katibu Mkuu wa UPAM Tanzania Joe Jolamu (kushoto) akingea na waandishi wahabari leo jijini Dar es salaam juu ya mashindano ya karate ya dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwakani. Kulia ni Rais wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina. R ais wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina akimshikilia shingo Master Hudu Thabit akionesha moja ya mbinu inazotumika kwa kujihami kwa ajili ya usalama. Rais wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina (kushoto) baada ya kuonesha mbinu ya kujihami kwa mwandishi wa habari Kibwana Dachi (aliyekaa). Kulia ni Master Hudu Thabit. Umoja wa Wapiganaji wa Sanaa ya Mapigano Duniani (UPAM) unaandaa shindano la kimataifa la wapiganaji ambalo linatarajiwa kufanyika nchini kati ya Mwezi Desemba mwaka huu na mwanzoni mwa mwaka ujao kutokana na ruhusa itakayotolewa na Serikali kwa mamlaka zinazohusika. Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa UPAM Prof. Maurizi Mardina alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar ...

TFF haitambui mabadiliko ya uongozi Coastal Union

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitambui mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika hivi karibuni. Uongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao tunautambua, na tutaendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine wowote ule. Tunapenda kuwakumbusha wanachama wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji. TFF inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu. Tayari tumepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake. Hivyo, tunafuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikishwa katika vyombo husika kwa hatua zaidi.

mwanariadha Montsho yupo mbioni kupigwa marufuku

Image
Mwanariadha bingwa wa zamani wa dunia wa mita 400 Amantle Montsho anakabiliwa na marufuku ya miaka miwili kutoshiriki michezo hiyo, baada ya kugundulika kutumia dawa za kuongeza nguvu wakati wa michezo ya Jumuia ya madola. Mwanariadha huyo wa Botswana mwenye umri wa miaka 31, ambaye alimaliza mashindano hayo kwa kuwa mshindi wa nne, anatakiwa mpaka Agosti 22 awe amekata rufaa katika Shirikisho la michezo ya Jumuia ya Madola CFG. Shirikisho hilo limeyapeleka matokeo ya vipimo hiyo kwa mashirikisho mengine ya michezo ya kimataifa, ambayo pia yanaweza kumpiga marufuku mwanariadha huyo kushiriki. Mike Hooper, Mkurugenzi mtendaji wa CFG, amesema mwanariadha huyo amejulishwa kuhusiana na matokeo ya vipimo hivyo na kwamba anahaki ya kuweza kujibu mpaka ifikapo Ijumaa Agosti 22. Shirikisho hilo linauwezo tu wa kubatilisha matokeo ya Montsho katika michezo hiyo, kufuatia kugundulika kutumia dawa. Iwapo atatiwa hat...

top 10 ya wasanii matajiri Africa

10. Jose Chameleone Jose (or Joe) Chameleone is a Ugandan artiste who found his niche blending traditional Ugandan folk music, a bit of rumba and a heavy reggae influence. He sings in English, Swahili and Luganda. His mansion outside of Kampala and four cars (including a Cadillac Escalade and a Benz) are evidence of his success, particularly with his hit, ValuValu. He's been credited with changing the face of music in Uganda, as well as making local music accessible to the rest of the world. 9. Banky W Born Olubankole Wellington in the U.S, Banky W moved back to Nigeria and grew up in Lagos, where he began singing at an early age. Finding success early in singing competitions, most of his wealth has come from endorsement deals with companies such as Etisalat mobile and Samsung in Nigeria. He also started the Mr Capable Foundation, an education charity that provides tuition scholarships for disadvantaged children. 8. Hugh Masekela Musical sensation Hug...

pesa nyingine hizoo daraja la kivukoni

Image
Waziri wa Ujenzi John Magufuli amesema Serikali inatarajia kuongeza kivuko kingine cha kuvusha watu Kigamboni ambacho kitagharimu shilingi bilioni 3.7 wakati ujenzi wa daraja ukiendelea. Anasema daraja linalojengwa sasa hivi litakamilika June 2015 badala ya July kama ilivyokua imefahamika mwanzoni ambapo tayari Mkandarasi ameshalipwa shilingi Bilioni 117 kati ya 214 za kukamilisha mradi wote limeandika gazeti la Tanzania Daima. Nalo gazeti la HabariLEO August 9 2014 limeandika >> Magufuli abana wenye magari Kigamboni, ataka wasisumbue abiria wa Pantoni asubuhi na jioni, wenye haraka watakiwa kuzunguka Kongowe – Mbagala, ni agizo la muda mfupi baada ya kivuko kilichopo kuzidiwa. chanzo millardayo.com

machache kuhusu Christian Bella

Image
  Jina lake halisi ni Christian Bella raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Bendi yake pia imekuwa maarufu lakini yeye ndiye anayevuma zaidi kutokana na kwamba kazi nyingi zinazofanya vizuri ni zake na hata asipokuwepo pengo linaonekana, wanaokwenda kwenye maonyesho ya bendi hiyo jijini Dar es Salaam hata mikoani watakuwa mashuhuda wa hilo. Ndiyo bendi ambayo kwa sasa inajaza zaidi kwenye maonyesho yake ukilinganisha na bendi nyingine ambazo ni maarufu na kongwe kuliko Malaika. Baadhi ya nyimbo za Bella zinazotamba kwa sasa ni ‘Nakuhitaji’, ‘Usilie’, ‘Msaliti’,‘Nani kama Mama’. Kikubwa kingine kilichombeba msanii huyo na bendi yake kwa sasa kuwa na nyimbo nyingi nzuri na zinazofahamika na mashabiki tofauti na bendi zingine. Lakini hata hivyo, rekodi inambeba msanii huyo kwa vile alipotua Akudo Impact alifanya vizuri na kung’ara na nyimbo alizotunga kama ‘Yako wapi Mapenzi’, ‘Bomoabomoa’ na ‘Safari Siyo Kifo’. “Kila mahali kuna changamoto zake, Aku...

Kinondoni kukamilisha ratiba ya Ligi ya Kikapu

KANDA ya Kinondoni ndio ya mwisho katika kukamilisha ratiba ya kupata timu nne zitakazoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA) inayotarajia kuanza mapema mwezi ujao. Rais wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), Richard Jules, alisema kuwa Kinondoni itaanza ligi yao leo Jumamosi ambayo itashirikisha timu nane. Alizitaja timu hizo kuwa ni Oilers, Pazi, Magnets, UDSM Outsiders, Crows, Mabibo Bullets, Don Bosco na Chui, wakati Kanda ya Temeke na Ilala tayari zilipata wawakilishi wake. “RBA msimu ujao itakuwa na timu 12 ambapo kila kanda itatoa timu nne, Temeke na Ilala walifanya ligi yao lakini Kinondoni hawakufanya kwa sababu ya kupisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. “Baadhi ya timu kutoka Temeke ni ABC na JKT Stars na Ilala ni Vijana na Savio wakati upande wa wanawake wao hawashiriki ligi ndogo kwa sababu timu zipo chache hivyo wanaingia moja kwa moja kwenye ligi,” alisema Jules.

picha za jana kwenye tamasha la matumaini 2014

Image
wasanii wa Maigizo,Cloud (kushoto) na JB, wakichana wakati wa Tamasha hilo. Jb alishinda kwa Pointi.  KWA MATUKIO KAMILI YA PICHA ZA TAMASHA HILI KAA NASI HAPO BAADAYE.     Msanii wa kunyanyua vitu vizito, Maisala Juma akionyesha umahiri wake wa kufanya mazoezi wakati wa Tamasha la Matumaini lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania katika kuazimisha sikukuu ya Nanenane katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Msanii wa muziki wa    nyimbo za dini    kutoka mbeya Bw. Ambwene Mwasongwe,akiimba na kukongonga nyoyo za mashabiki wa nyimbo zake wakati wa Tamasha la Matumaini lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania katika kuazimisha sikukuu ya    Nanenane katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Kikosi cha Bongo Movie kilichokikabili kikosi cha Bongo wakati wa Tamasha la Matumaini lililoandaliwa na Global Publishers na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania katika kuazimisha sikukuu ya    Nanenane katika Uwanja ...