Hii ndio sababu ya Diddy kumpiga Drake


Tmz imeripoti kuwa wimbo uliomfanya Drake apigwe na Puff Daddy ni “0 to 100/ The Catch Up” ambao mpaka sasa umetajwa kuwania tuzo mbili za Grammy kama Best Rap Performance na Best Rap Song.
Diddy aligombana na Drake jumatatu asubuhi baada ya sherehe ya siku ya kuzaliwa na Dj Khaled nje ya club ya LIV huko Miami Beach na sababu ikiwa Diddy alihisi amekosewa heshima na Drake.

Producer maarufu Boi-1da aliwapa Diddy na Drake wimbo huu ili warekodi miezi nane iliyopita ila Drake alikwenda kurekodi wimbo huu mwenyewe bila kumwambia Pdd kitu ambacho kilimkasirisha Pdd.

Diddy alimuona Drake nje ya Club LIV nakuamua kuzungumza naye ndipo Drake alionyesha madharau, kabla hajampiga Pdd alimwambia “Hutokaa kunikosea heshima tena” “You’ll never disrespect me again” .

Comments

Popular posts from this blog

soma habali za kwenye magazeti leo

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z