Posts

Showing posts from February, 2015

Stala thomas afumaniwa

Image
Stori: Deogratius Mongela na Chande Abdallah/Risasi HAYA ni madai mazito! Kwamba, staa wa Bongo Fleva ambaye juzikazti alinusa kwenye gospo ‘ikamshinda', Stara Thomas anadaiwa kufumaniwa na mumewe, Raumu Ally mpaka kufikishana polisi, Risasi Jumamosi halipitwagi na ‘ubuyu’. Staa wa Bongo Fleva, Stara Thomas akiwa na mumewe. Kwa mujibu wa shuhuda wa kuaminika, tukio hili lilijiri hivi karibuni nyumbani kwa familia hiyo, Tabata jijini Dar es Salaam. FUMANIZI LILIVYOTOKEA Akilisimulia… Stori: Deogratius Mongela na Chande Abdallah/Risasi HAYA ni madai mazito! Kwamba, staa wa Bongo Fleva ambaye juzikazti alinusa kwenye gospo ‘ikamshinda', Stara Thomas anadaiwa kufumaniwa na mumewe, Raumu Ally mpaka kufikishana polisi, Risasi Jumamosi halipitwagi na ‘ubuyu’. Staa wa Bongo Fleva, Stara Thomas akiwa na mumewe. Kwa mujibu wa shuhuda wa kuaminika, tukio hili lilijiri hivi karibuni nyumbani kwa familia hiyo, Tabata jijini Dar es

Boko Haram waondoka Gombe

Wapiganaji Waislamu wa Boko Haram wametoka katika mji wa Gombe kaskazini-mashariki mwa Nigeria baada ya mapambano makali na jeshi. Wakuu wanasema wapiganaji wamerejeshwa nyuma, lakini ripoti nyengine zinasema kuwa wapiganaji hao waliondoka kwa hiari yao. Boko Haram waliingia Jumamosi asubuhi katika vitongoje vya Gombe baada ya kushambulia mji jirani wa Dadin Kowa. Wapiganaji hao wamewahi kufanya mashambulio ya kujitolea mhanga katika mji wa Gombe, lakini hawakupata kujaribu kuuteka mji wenyewe. Nigeria ikitarajiwa kufanya uchaguzi tarehe 14 Februari, lakini umeakhirishwa kwa majuma sita kwa sababu ya wasiwasi kuhusu usalama.

Zuma: hakuna ruhusa mgeni kumiliki ardhi

Wageni hawatoruhusiwa kumiliki ardhi Afrika Kusini, kufuatana na sheria kali zinazopendekezwa na Rais Jacob Zuma. Siku zijazo wageni wataruhusiwa tu kukodi kwa muda mrefu ardhi ya mashamba ya Afrika Kusini. Mbali ya hayo, mtu yeyote anayemiliki zaidi ya hekta 12,000 atalazimishwa kuiuzia serikali ili ipate kugawiwa. Ardhi bado ni swala linalozusha hamasa nchini humo - ambako karne tatu za ukoloni na ubaguzi wa rangi - zimeacha ardhi nyingi mikononi mwa wachache, hasa wazungu. Tangu kumalizika ubaguzi wa rangi mwaka 1994, chama tawala cha ANC, kimeshindwa kufikia lengo lake la kugawa thuluthi ya ardhi ya kilimo kwa Waafrika, ulipofika mwaka 2014 chanzo bbc