Boko Haram waondoka Gombe
Wapiganaji Waislamu wa Boko Haram
wametoka katika mji wa Gombe kaskazini-mashariki mwa Nigeria baada ya
mapambano makali na jeshi.
Wakuu wanasema wapiganaji wamerejeshwa nyuma, lakini ripoti nyengine zinasema kuwa wapiganaji hao waliondoka kwa hiari yao.Boko Haram waliingia Jumamosi asubuhi katika vitongoje vya Gombe baada ya kushambulia mji jirani wa Dadin Kowa.
Wapiganaji hao wamewahi kufanya mashambulio ya kujitolea mhanga katika mji wa Gombe, lakini hawakupata kujaribu kuuteka mji wenyewe.
Nigeria ikitarajiwa kufanya uchaguzi tarehe 14 Februari, lakini umeakhirishwa kwa majuma sita kwa sababu ya wasiwasi kuhusu usalama.
Comments
Post a Comment