Zuma: hakuna ruhusa mgeni kumiliki ardhi

Wageni hawatoruhusiwa kumiliki ardhi Afrika Kusini, kufuatana na sheria kali zinazopendekezwa na Rais Jacob Zuma.
Siku zijazo wageni wataruhusiwa tu kukodi kwa muda mrefu ardhi ya mashamba ya Afrika Kusini.
Mbali ya hayo, mtu yeyote anayemiliki zaidi ya hekta 12,000 atalazimishwa kuiuzia serikali ili ipate kugawiwa.
Ardhi bado ni swala linalozusha hamasa nchini humo - ambako karne tatu za ukoloni na ubaguzi wa rangi - zimeacha ardhi nyingi mikononi mwa wachache, hasa wazungu.
Tangu kumalizika ubaguzi wa rangi mwaka 1994, chama tawala cha ANC, kimeshindwa kufikia lengo lake la kugawa thuluthi ya ardhi ya kilimo kwa Waafrika, ulipofika mwaka 2014

chanzo bbc

Comments

Popular posts from this blog

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z

mbinu za kuwa producer au mtayarishaji wa music