Posts

Showing posts from September, 2014

Ukawa wamtia kitanzi Sitta

Image
UAMUZI uliofikiwa na viongozi wa vyama vya siasa na Rais Jakaya Kikwete umemweka katika wakati mgumu Mwenyeki wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta kuahirisha au la vikao vya Bunge hilo. Hii inafuatia Rais Kikwete na viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kukubaliana kusitisha Bunge la Katiba Oktoba 4 tofauti na ratiba ya Sitta ambayo inaonyesha vikao vitaendelea hadi Oktoba 31 atakapomkabidhi rais katiba iliyopendekezwa. Vilevile kwa tafsiri ya uamuzi huo, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) watakuwa wameibuka kidedea kwani tangu mwanzo walikuwa wanataka Bunge hilo liahirishwe hadi maridhiano yapatikane. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo, alisema katika makubaliano ya kikao chao na rais kilichofanyika juzi Ikulu ndogo mjini hapa, walikubaliana kwa pamoja kuwa Bunge la Katiba liendelee hadi Oktoba 4. Kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa imetolewa mara baada ya awamu ya pili ya Bunge la Katiba kuanza Oktoba 10 hadi 21, ndiyo waju

Dk. Slaa asema hana barua ya msajili

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema hajawahi kupokea barua yoyote kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, inayowataka waitishe mkutano wa Kamati Kuu ili kufanya marekebisho ya Katiba yao. Wakati Dk. Slaa anatoa kauli hiyo, Julai, mwaka huu, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa chama hicho, John Mnyika, alizungumza na vyombo vya habari kuwa Agosti, 2006 walifanya marekebisho makubwa ya Katiba ikiwamo kifungu kilichokuwa kinaweka ukomo wa uongozi. Juzi, Jaji Mutungi akizungumza na gazeti hili, alieleza kuwa kinachotokea sasa ndani ya chama hicho ni matokeo ya kupuuzwa ushauri wake wa kukitaka kifanye marekebisho ya Katiba yake. Kauli za viongozi hao zilitokana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwekewa pingamizi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Tabora, Kansa Mbarouk, ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya uenyekiti taifa, akidai chama chake kimekiuka Katiba na maagizo ya msajili. Barua ya Msajili wa Vyama

WAZIRI WA AFYA NA NAIBU WAKE WATEMBELEA HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA, ZANZIBAR

Image
Waziri wa Afya Mh. Rashid Seif akiongozana na Naibu wake Mh. Mahmoud Thabit Kombo wakitembelea eneo la Hospitali ya Mnzammoja katika ziara yake ya kutembelea Hospitali hiyo. Mkuu wa kitengo cha maradhi ya kisukari katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja Dkt Miskia Ali akitowa maelezo kwa Waziri wa Afya juu ya kadhia ya maradhi hayo. Waziri wa Afya akipata maelezo ya shughuli za Maabara kutoka kwa mtaalamu wa Maabara wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Marijani.

Mtoto wa Obasanjo apigwa risasi Nigeria

Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olesugun Obasanjo amejeruhiwa kwa risasi wakati wa mapambano na wanamgambo wa kiislamu Boko Haram. Luteni Kanali Adeboye Obasanjo alijeruhiwa siku ya jumatatu wakati jeshi la Nigeria lilipokuwa likipambana kuudhibiti mji wa Michika karibu na mji wa Mubi mji uliokuwa ukidhibitiwa na wanamgambo katika jimbo la Adamawa. Msemaji wa zamani wa Olusegun Obasanjo ameiambia BBC kuwa kanali Adeboye anaendela vizuri. Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao, wanajeshi wameondoka kwenye kambi za kijeshi na chuo katika jimbo hilo kufungwa. Wanamgambo wa Boko haram wamedhibiti miji mingi kaskazini mashariki na kutangaza kuwa himaya za kiislamu

Mlipuko waua viongozi wa waasi Syria

Wanachama 50 wa kundi moja la waasi wa Syria wameuawa au kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga. Vyombo vya habari vya serikali na wanaharakati wanasema mshambuliaji wa kujilipua aliilenga nyumba moja katika jimbo la Idlib, ambamo viongozi wa Ahrar al-Sham walikuwa wakikutana. Kamanda wa kikundi hicho Hassan Abboud ni miongoni mwa watu waliouawa. Kiongozi huyo ameuawa pamoja na makamanda wengine wa ngazi za juu wa kikundi hicho. Shambulio hilo limefanywa na mtu aliyejilipua katika mji wa Ram Hamdan kaskazini magharibi mwa Syria. Ahrar al Sham ni sehemu ya kikundi cha Islamic State, muungano wa vikundi saba vya waasi wa kiislamu nchini Syria.