Mtoto wa Obasanjo apigwa risasi Nigeria

Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olesugun Obasanjo amejeruhiwa kwa risasi wakati wa mapambano na wanamgambo wa kiislamu Boko Haram.

Luteni Kanali Adeboye Obasanjo alijeruhiwa siku ya jumatatu wakati jeshi la Nigeria lilipokuwa likipambana kuudhibiti mji wa Michika karibu na mji wa Mubi mji uliokuwa ukidhibitiwa na wanamgambo katika jimbo la Adamawa.

Msemaji wa zamani wa Olusegun Obasanjo ameiambia BBC kuwa kanali Adeboye anaendela vizuri.

Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao, wanajeshi wameondoka kwenye kambi za kijeshi na chuo katika jimbo hilo kufungwa.

Wanamgambo wa Boko haram wamedhibiti miji mingi kaskazini mashariki na kutangaza kuwa himaya za kiislamu

Comments

Popular posts from this blog

soma habali za kwenye magazeti leo

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z