Mlipuko waua viongozi wa waasi Syria
Wanachama 50 wa kundi moja la waasi wa Syria wameuawa au kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga.
Vyombo
vya habari vya serikali na wanaharakati wanasema mshambuliaji wa
kujilipua aliilenga nyumba moja katika jimbo la Idlib, ambamo viongozi
wa Ahrar al-Sham walikuwa wakikutana.Kamanda wa kikundi hicho Hassan Abboud ni miongoni mwa watu waliouawa.
Kiongozi huyo ameuawa pamoja na makamanda wengine wa ngazi za juu wa kikundi hicho. Shambulio hilo limefanywa na mtu aliyejilipua katika mji wa Ram Hamdan kaskazini magharibi mwa Syria.
Ahrar al Sham ni sehemu ya kikundi cha Islamic State, muungano wa vikundi saba vya waasi wa kiislamu nchini Syria.
Comments
Post a Comment