Muhubiri awabaka wanawake akidai kuwaponya
Muhubiri wa zamani aliyedai kuwa na
'nguvu za kuponya' amepewa adhabu ya kifungo cha nje cha miaka ishiriki
kwa kumyanyasa kimapenzi mwanamke mmoja nchini Australia.
Muhubiri
huyo alidai kutumia kile alichokiita 'nguvu za kipekee' za uponyaji
kumdhalilisha kimapenzi mwanamke huyo akisema kuwa alikuwa na mashetani
katika sehemu yake ya siri.Omar Sheriff, mwenye umri wa miaka 67, alimwambia mwanamke huyo mnamo mwaka 1994 kwamba alikuwa na mashetani mwilini mwake na kwamba mashetani hayo yalipaswa kuondolewa kwa njia maalum katika kiwanda chake cha fanicha mtaani Campbellfield.
Kwa mujibu wa taarifa za jarida la 'The Age', jaji Jane Patrick alifahamishwa kuwa Omar alidai alikuwa na nguvu kubwa sana za kimiujiza na alimuonya mwanamke huyo aliyekuwa na miaka 30 kwamba angefariki ikiwa mashtenai hayo hayangetolewa kutoka katika sehemu yake ya siri.
Alisema alikuwa na utabiri kuhusu maisha yake na kumwambia kuwa angepata shida kubwa sana ikiwa asingetolewa mashteni hayo.
Sheriff aliwahi kufungwa jela mwaka 1997 kwa miaka minane lakini adhabu yake ilipunguzwa hadi miaka sita kwa kosa la kuwabaka wanawake watatu kwa madai hayo hayo.
Shariff hakumbaka tu mwanamke huyo bali wanawake wengine watatu.
Jaji alimwambia Sheriff kwamba wanawake hao waliokuja kwake na matatizo ya kindoa walimwamini sana kwamba angewasaidia lakini wao ndio walikuwa waathiriwa wa kwanza wa upuzi wa ''nguvu zake za kimiujiza''
Sheriff alikiri makosa matatu ya kuwaingilia kimwili wanawake kwa kuwahadaa, makosa aliyoyafanya kati ya Januari na Disemba mwaka 1994.
Mahakama iliambiwa kuwa baada ya muhubiri huyo kuwabaka wanawake hao aliwaambia waje na chupa ya Coca-Cola, mayani na ubavu wa nyama ya Kondoo.
Alikuwa anawaingiza ndani ya nyumba yake na kuwapeleka katika chumba chake ambako aliwatendea unyama huo mara kwa mara.
Katika hukumu yake Jaji Patrick alisema kuwa Sheriff, anakabiliwa na matatizo ya kiafya na changamoto za kisaikolojia na kwamba kwa sababu alikiri makosa basi ameoneolea waathiriwa wake uchungu wa kuanza kutoa ushahidi.
Comments
Post a Comment