baiskeli ya dhahabu yazinduliwa Uingereza, bei yake ni sh.milion 676.5

NI rahisi sana kwa watu kulalamikia gharama ya kununua baisekli wengi wakitaka bei nafuu. Baiskeli nyingi nchini Uingereza huuzwa kwa pauni 1,000 sawa na shilingi milioni 2.7 za Tanzania ambazo kwa watu wengi nchini humo ni fedha nyingi sana. Hata hivyo baiskeli mpya iliyotengezwa kwa dhahabu imezinduliwa nchini humo. Bei yake? Pauni 250,000 sawa na milioni 676.5 za Tanzania. Bei hii ni ghali hata kuliko bei ya gari jipya aina ya Ferari.
Baiskeli hiyo imetengenezwa na kampuni ambayo hutengeza vitu vya kifahari, Goldgenie na imetengezwa kwa dhahabu.Kiwango cha dhahabu iliyotumiwa ni karati 24. Wataalamu wa kampuni hiyo ya Goldgenie, wameweka dhahabu katika vyuma vya baiskeli hiyo vyote ikiwemo mnyororo na mfumo unaofanya baiskeli kwenda na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu.

Mkurugenzi wa kampuni iliyotengeza baiskeli hii anasema inaweza kuendeshwa katika barabara kama baiskeli nyinginezo.
Source: BBC

Comments

Popular posts from this blog

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z

mbinu za kuwa producer au mtayarishaji wa music