Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amewataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaounda kamati hiyo, kufanya kazi kama ilivyo kamati yake kwa Tanzania Bara.
Zitto aliyasema hayo jana kwenye semina ya wawakilishi hao iliyofanyika jijini hapa ambapo alisema, kamati husimamia matumizi yote ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoidhinishwa na baraza na kutoa taarifa zake kwa Umma.
Alisema hesabu za Serikali huendana na Ripoti ya CAG ambayo ndiyo nyenzo kuu ya Baraza katika kusimamia fedha za umma.
Hata hivyo, Zitto alisema PAC inapoona inafaa, huagiza ukaguzi maalumu kwenye maeneo mahususi na njia hiyo imesaidia kuibuliwa kwa mambo mengi ya ufisadi wa fedha za umma kwa Tanzania Bara.
“Kuna nyakati mkaguzi anakuwa haoni masuala fulani hadi anapoombwa na vyombo vingine na hata wananchi…Ni vyema Kamati ya PAC Zanzibar kutumia pia njia hii ili kuimarisha usimamizi bora wa fedha za umma kwa Zanzibar kama ilivyo sasa katika Jamhuri ya Muungano,” alisema Zitto na kuongeza;
“Ni muhimu kuzingatia kwamba wawakilishi ndiyo chombo cha mwisho katika uamuzi kuhusu masuala ya wananchi wa Zanzibar ikiwamo matumizi ya fedha za umma.”
Ni muhimu kuhakikisha kuwa Wizara ya Fedha ya Zanzibar inajibu hoja za PAC (treasury notes) na hapo ndipo mzunguko wa uwajibikaji unakuwa umekamilika.
Alisema ni wakati wa kufikiria namna ambavyo CAG na PAC wanaweza kutimiza wajibu wao katika kuzuia matumizi yanayoelekea kutokuwa na ufanisi.
chanzo:mwananchi

Comments

Popular posts from this blog

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z

mbinu za kuwa producer au mtayarishaji wa music