machache kuhusu Christian Bella
Jina lake halisi ni Christian Bella raia wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Bendi yake pia imekuwa maarufu
lakini yeye ndiye anayevuma zaidi kutokana na kwamba kazi nyingi
zinazofanya vizuri ni zake na hata asipokuwepo pengo linaonekana,
wanaokwenda kwenye maonyesho ya bendi hiyo jijini Dar es Salaam hata
mikoani watakuwa mashuhuda wa hilo.
Ndiyo bendi ambayo kwa sasa inajaza zaidi kwenye
maonyesho yake ukilinganisha na bendi nyingine ambazo ni maarufu na
kongwe kuliko Malaika.
Baadhi ya nyimbo za Bella zinazotamba kwa sasa ni
‘Nakuhitaji’, ‘Usilie’, ‘Msaliti’,‘Nani kama Mama’. Kikubwa kingine
kilichombeba msanii huyo na bendi yake kwa sasa kuwa na nyimbo nyingi
nzuri na zinazofahamika na mashabiki tofauti na bendi zingine.
Lakini hata hivyo, rekodi inambeba msanii huyo kwa
vile alipotua Akudo Impact alifanya vizuri na kung’ara na nyimbo
alizotunga kama ‘Yako wapi Mapenzi’, ‘Bomoabomoa’ na ‘Safari Siyo Kifo’.
“Kila mahali kuna changamoto zake, Akudo kulikuwa na changamoto
ambazo naweza kukumbana nazo sehemu nyingine, hivyo ni jambo la kawaida,
naweza kusema kwamba niliondoka Akudo bila kugombana na mtu, nilitaka
kuendesha mambo yangu mwenyewe,” anaeleza Bella katika mahojiano maalumu
kwenye ofisi za Mwanaspoti, Tabata Relini jijini Dar es Salaam.
“Mwaka 2012 nilienda Sweden kwa mke wangu ambaye
alikuwa anajifungua hivyo nililazimika kuwepo ili kushuhudia mtoto wangu
akizaliwa, nilishuhudia kila kitu na sasa nina watoto wawili wa kiume
Jordan (7) na Hance (2).
“Nikiwa huko nilitunga wimbo ulioitwa ‘Msaliti’
ambao niliutuma hapa nchini na ulifanya vizuri, niliporudi nikawa
mwanamuziki wa kujitegemea na kupata shoo zote za Fiesta ambapo
mwanamuziki wa dansi nilikuwa peke yangu,” anaongeza.
Chanzo cha wimbo wa Nani Kama Mama
“Niliamua kutunga wimbo huu baada ya kushuhudia
hatua zote mke wangu alipojifungua, kiukweli mwanamke anatakiwa
kuheshimika tofauti na wanavyowachukulia, hapo ndipo niliona kuna haja
ya kuimba wimbo wenye ujumbe huu.
“Hata katika uzinduzi wangu nimeupa jina la Usiku
wa Mama ni maalumu kwa akina mama wote duniani, uzinduzi ambao
nitaufanya Mzalendo Pub, Agosti 29, mwaka huu,” anasema Bella ambaye
katika wimbo huo amemshirikisha Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz.
Comments
Post a Comment