Ghana ipo kwenye hatari ya kupigwa marufuku ya FIFA

Ghana inakabiliwa na tishio la kupigwa marufuku na shirikisho la soka duniani FIFA baada ya serikali kuanzisha uchunguzi wa matokeo duni katika kombe la dunia huko Brazil.
The Black stars ya Ghana ilimaliza na alama moja pekee katika kundi G baada ya kucheza mechi tatu .

Aidha kampeini yao huko Brazil ilikumbwa na misukosuko ya nidhamu na migomo ya malimbikizi ya marupurupu ya wachezaji.
FIFA imeipatia onyo shirikisho la soka la Ghana kuikumbusha kuwa inakiuka kanuni za shirikisho hilo kwa kuruhusu au kushiriki uchunguzi wa aina yeyote kuhusiana na matokeo duni katika mchuano wa kombe la dunia huko Brazil.




Muntari na Boateng wakijivinjari baada ya kutimuliwa kambini
Kwa wakati mmoja rais wa Ghana John Mahama alilazimika kuingilia kati na kutuma zaidi ya dola milioni tatu za Marekani ilikuzuia mgomo wa wachezaji kufuatia malimbikizi ya marupurupu.
Rais Mahama baadaye aliagiza uchunguzi wa kina ufanywe ilikubaini kwa nini Ghana ilishindwa kusajili matokeo mazuri .
Hata hivyo FIFA inaharamisha kuingiliwa kati kwa mashirika ya soka na mtu yeyote ima ni serikali wala yeyote.
Katika barua hiyo iliyotiwa sahihi na naibu katibu mkuu wa FIFA Markus Kattner uchunguzi huo wa serikali unakiuka sheria na kanuni za uhuru wa vyama shirika.
Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Ghana kushindwa kufuzu kwa mkondo wa pili.
Ghana ilitoka sare ya 2-2 na Ujerumani huko Fortaleza,kabla ya kuambulia kichapo dhidi ya Marekani na Ureno.
Wachezaji Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng walitimuliwa kambini kwa utovu wa nidhamu.

Comments

Popular posts from this blog

soma habali za kwenye magazeti leo

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z