mwanariadha Montsho yupo mbioni kupigwa marufuku

Mwanariadha bingwa wa zamani wa dunia wa mita 400 Amantle Montsho anakabiliwa na marufuku ya miaka miwili kutoshiriki michezo hiyo, baada ya kugundulika kutumia dawa za kuongeza nguvu wakati wa michezo ya Jumuia ya madola.
Mwanariadha huyo wa Botswana mwenye umri wa miaka 31, ambaye alimaliza mashindano hayo kwa kuwa mshindi wa nne, anatakiwa mpaka Agosti 22 awe amekata rufaa katika Shirikisho la michezo ya Jumuia ya Madola CFG.
Shirikisho hilo limeyapeleka matokeo ya vipimo hiyo kwa mashirikisho mengine ya michezo ya kimataifa, ambayo pia yanaweza kumpiga marufuku mwanariadha huyo kushiriki.
Mike Hooper, Mkurugenzi mtendaji wa CFG, amesema mwanariadha huyo amejulishwa kuhusiana na matokeo ya vipimo hivyo na kwamba anahaki ya kuweza kujibu mpaka ifikapo Ijumaa Agosti 22.
Shirikisho hilo linauwezo tu wa kubatilisha matokeo ya Montsho katika michezo hiyo, kufuatia kugundulika kutumia dawa.
Iwapo atatiwa hatiani, Montsho atapelekwa katika Shirika la Kimataifa la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu michezoni WADA, pamoja na mashirika maengine kwa ajili ya kukabiliwa na vikwazo zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

soma habali za kwenye magazeti leo

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z