Kinondoni kukamilisha ratiba ya Ligi ya Kikapu
KANDA ya Kinondoni ndio ya mwisho katika kukamilisha ratiba ya
kupata timu nne zitakazoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es
Salaam (RBA) inayotarajia kuanza mapema mwezi ujao.
Rais wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es
Salaam (BD), Richard Jules, alisema kuwa Kinondoni itaanza ligi yao leo
Jumamosi ambayo itashirikisha timu nane.
Alizitaja timu hizo kuwa ni Oilers, Pazi, Magnets,
UDSM Outsiders, Crows, Mabibo Bullets, Don Bosco na Chui, wakati Kanda
ya Temeke na Ilala tayari zilipata wawakilishi wake.
“RBA msimu ujao itakuwa na timu 12 ambapo kila
kanda itatoa timu nne, Temeke na Ilala walifanya ligi yao lakini
Kinondoni hawakufanya kwa sababu ya kupisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan.
“Baadhi ya timu kutoka Temeke ni ABC na JKT Stars
na Ilala ni Vijana na Savio wakati upande wa wanawake wao hawashiriki
ligi ndogo kwa sababu timu zipo chache hivyo wanaingia moja kwa moja
kwenye ligi,” alisema Jules.
Comments
Post a Comment