mashindano ya karate ya dunia kufanyika Tanzania
Katibu
Mkuu wa UPAM Tanzania Joe Jolamu (kushoto) akingea na waandishi
wahabari leo jijini Dar es salaam juu ya mashindano ya karate ya dunia
yanayotarajiwa kufanyika nchini mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni
mwakani. Kulia ni Rais wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina.
Rais
wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina akimshikilia shingo Master Hudu
Thabit akionesha moja ya mbinu inazotumika kwa kujihami kwa ajili ya
usalama.
Rais
wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina (kushoto) baada ya kuonesha mbinu
ya kujihami kwa mwandishi wa habari Kibwana Dachi (aliyekaa). Kulia ni
Master Hudu Thabit.
Umoja wa Wapiganaji wa Sanaa ya
Mapigano Duniani (UPAM) unaandaa shindano la kimataifa la wapiganaji
ambalo linatarajiwa kufanyika nchini kati ya Mwezi Desemba mwaka huu na
mwanzoni mwa mwaka ujao kutokana na ruhusa itakayotolewa na Serikali kwa
mamlaka zinazohusika.
Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa UPAM Prof. Maurizi Mardina alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
Profesa Mardina amesema kuwa
mchezo wa kupigana ni mchezo mzuri ambao unahitaji kujitoa na uwezo
mzuri wa kufikiri na siyo mchezo au mafunzo yanayosababisha uonevu bali
ni mafunzo yanayompa mtu uwezo wa kujilinda na kujitetea.
Ameongeza kwa kusema kuwa Nchi 102
zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watashiriki wachezaji 25
wa umri na jinsia zote kutoka katika nchi hizo.
“Walimu wanafundisha vizuri ili
kuandaa timu bora na baadhi ya vifaa tayari vimenunulia vyenye thamani
ya dola ya kimarekani 25000.” amesema Mardina.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
UPAM Tanzania Joe Jolamu ameeleza kuwa mashindano ya ndani tayari
yameishaanza na yanaendelea ili kuweza kupata timu moja ya taifa
itayocheza katika mashindano ya dunia.
“Wachezaji ambao wataruhusiwa
kujiunga na kuingia katika kuchezea timu ya dunia ni wale tu ambao wapo
katika kikosi maalumu” alisema mwalimu
Aidha, mmoja wa wanafunzi wa
mchezo huo Hafidhi Kunambi anayepata mafunzo ya mchezo huo ameonesha
jinsi alivyojifunza namna ya kujilinda kadiri ya mafunzo aliyopata.
Kwa Tanzania wanatakiwa washiriki
45 ambao wamefanya mazoezi ili kuweza kushiriki mashindano hayo kutoka
maeneo mbalimbali nchini na kupata timu bora itakayoleta ushindi.
Comments
Post a Comment