TFF haitambui mabadiliko ya uongozi Coastal Union
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) halitambui mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal Union
yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika
hivi karibuni.
Uongozi wa Coastal Union
uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao
tunautambua, na tutaendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine
wowote ule.
Tunapenda kuwakumbusha wanachama
wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba
zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za
utendaji. TFF inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa
njia ya uchaguzi tu.
Tayari tumepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake.
Hivyo, tunafuatilia suala hilo kwa
kina, na ikibainika kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo
watafikishwa katika vyombo husika kwa hatua zaidi.
Comments
Post a Comment