RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKTABA YAKIRAIS YA GEORGE W. BUSH JIJINI DALLAS, TEXAS
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) iliyo katika Taasisi ya Bush (George W. Bush Institute) mjini Dallas, Texas, na kujionea nafasi kubwa iliyotolewa kwa Tanzania na zawadi ambazo Rais Bush alizipata katika ziara yake rasmi ya Tanzania wakati akiwa Rais wa Marekani.
Maktaba hiyo ya
kuvutia inaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa kabisa ya habari na
mawasiliano.
Rais Kikwete alikuwa amesimama mjini Dallas kwa muda akiwa njiani kutoka
Washington D.C., kwenda Houston, jimbo hilo hilo la Texas kuhudhuria
mkutano wa wafanyabiashara wa mafuta na gesi ambao wanataka kuwekeza katika
sekta hiyo katika Tanzania.
Rais Kikwete amekuwa katika Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku tisa,
ambako miongoni mwa mambo mengine, amehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za
Marekani na Afrika uliofikia kilele chake jana kwa kikao kilichoendeshwa na
Rais Barack Obama wa Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani
mjini Washington D.C.
b1: Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library) sehemu ambayo imejengwa kwa mfano wa Ikulu ya Marekani, White House, hususan katika bustani ya Waziri (Rose Garden) pamoja na ofisi ya Rais wa Marekani, Oval office*
*b3, b4, b5: *Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library) *

*b3, b4, b5: *Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiondoka baada ya kutembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library)
Comments
Post a Comment