MTOTO WA R KELLY ASISAMUA WATU BAADA YA KUTAKA KUBADILI JINSIA


Mtoto wa mwanamuziki mkongwe wa R&B wa nchini Marekani R Kelly ametangaza kubadilisha jinsia yake kupitia mitandao ya kijamii.

Mtoto JAYA alizaliwa mwanamke lakini akachukua uamuzi mgumu na kuwaambia mashabiki kuwa sasa hivi yeye ni mwanaume na jina lake ni JAY kwakuwa amebadilisha jinsia yake.

Lakini wakati mama yake Andrea Kelly akimuunga mkono mtoto wake kutokana na hatua hiyo, baba yake R Kelly bado hajazungumza chochote na mashabiki wa R Kelly wanasubilia kwa hamu kauli yake kuhusu maamuzi ya mtoto wake.
 Jay amesema mama yake alifurahishwa sana kwa kitendo chake hicho na kusema anampenda mtoto wake vyovyote vile alivyo ambapo anamshukuru mama yake kwa kukubali yeye kubadili jinsia yake na kuwa mwanaume.
 Pia ameongeza kuwa anaamini yeye sasa ni mwanaume na anataka upasuaji zaidi na tiba ya kumsaidia kuwa vile alivyotakiwa.
Jay amesema akiwa na umri wa miaka sita alijigundua kuwa anavutiwa sana na wasichana lakini hataki mahusiano kwanza.

Comments

Popular posts from this blog

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z

mbinu za kuwa producer au mtayarishaji wa music