HATIMAYE DAVIDO AWA MSHINDI WA TUZO ZA BET

 Screen Shot 2014-06-29 at 9.07.09 PM


Hii ilikua siku nyingine muhimu kwa Tanzania na Africa kwa ujumla ambapo yalikua yanasubiriwa matokeo ya tuzo ya BET sanasana kipengele wanachowania tuzo wasanii wa Afrika akiwemo Diamond Platnumz.
Davido kutoka Nigeria ndio amethibitisha kuwa mshindi wa tuzo hii ambapo kupitia page yake ya Instagram amewashukuru mashabiki na kuelezea furaha yake.
Tuzo hii ilikua inawaniwa na Diamond Platnumz kutoka Tanzania, Mafikizolo wa South Africa, Sarkodie wa Ghana, Tiwa Savage wa Nigeria na Toofan wa Togo.
Pamoja na kwamba Diamond hajawa mshindi wa tuzo hii, Watanzania wengi wamekua upande wake toka alipochaguliwa kuwania tuzo hizi na kumwambia hata kama hatoshinda, kuchaguliwa tu kushiriki BET ni zawadi ya kipekee na hatua kubwa kimuziki.
Namkariri Rais Jakaya Kikwete pia aliesema ‘Hata kama asiposhinda Diamond, yenyewe kuchaguliwa kwenye tuzo za BET ni hatua kubwa kimuziki’
Screen Shot 2014-06-29 at 9.07.17 PM

Comments

Popular posts from this blog

soma habali za kwenye magazeti leo

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z