Posts

Showing posts from June, 2014

DAIMOND SASA NI LEVO ZA KIMATAIFA HEBU CHEKI PICHA HIZI

Image
aisee noma sanaaaa

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA DAIMOND BAADA YA KUKOSA TUZO YA BET

Image
baada ya kushindwa kupata tuzo ya BET daimond ameandika hivi kwenye mitandao ya kijamii ‘Tusipopenda kukubali matokeo na ushindi wa wenzetu basi daima hatutaweza kuwa washindani, muhimu ni kujua wapi tulipotoka na wapi tulipo leo, katika nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya milioni 40 kuchaguliwa Tanzania ni fursa, heshima na hatua kubwa, cha muhimu ni kuitumia vyema fursa hii na kuhakikisha mwakani tunapiga hatua, asante sana kwa wote wanaozidi kunisupport’

HATIMAYE DAVIDO AWA MSHINDI WA TUZO ZA BET

Image
  Hii ilikua siku nyingine muhimu kwa Tanzania na Africa kwa ujumla ambapo yalikua yanasubiriwa matokeo ya tuzo ya BET sanasana kipengele wanachowania tuzo wasanii wa Afrika akiwemo Diamond Platnumz. Davido kutoka Nigeria ndio amethibitisha kuwa mshindi wa tuzo hii ambapo kupitia page yake ya Instagram amewashukuru mashabiki na kuelezea furaha yake. Tuzo hii ilikua inawaniwa na Diamond Platnumz kutoka Tanzania, Mafikizolo wa South Africa, Sarkodie wa Ghana, Tiwa Savage wa Nigeria na Toofan wa Togo. Pamoja na kwamba Diamond hajawa mshindi wa tuzo hii, Watanzania wengi wamekua upande wake toka alipochaguliwa kuwania tuzo hizi na kumwambia hata kama hatoshinda, kuchaguliwa tu kushiriki BET ni zawadi ya kipekee na hatua kubwa kimuziki. Namkariri Rais Jakaya Kikwete pia aliesema ‘Hata kama asiposhinda Diamond, yenyewe kuchaguliwa kwenye tuzo za BET ni hatua kubwa kimuziki’

KABURI LILILOVUNJA REKODI YA DUNIA MAITI YAWEKEWA KITANDA NK.

Image
Kiboko cha yaote mtu aliyezikwa katika kaburi lililotengenezwa kama chumba cha kulala kilicho na samani tofauti za thamani kubwa sana kama vile flat screen, dreassing table, kitanda na vitu vingine vingi mpaka mvinyo, perfumes na vingine vingi, hii ndio top katika dunia hii, angalia picha zaidi za tukio hilo.

kali ya mwaka afanyiwa operation (upasuaji) akiwa anaimba

Image
Mwimbaji Alama Kante ametoa mshangao wa mwaka baada ya kulazimika kuimba huku akifanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kwenye koo lake ili madaktari wasiharibu sauti yake. Mwimbaji huyo kutoka Guinea mwenye makazi yake nchini Ufaransa alipatiwa dawa za kumfanya asisikie maumivu wala uchungu wakati wote wa zoezi la upasuaji. Kante alikuwa akiogopa kupoteza sauti yake lakini daktari wake alipendekeza afanyiwe upasuaji huku anaimba. Kante ambaye kwa sasa amepata nafuu amesema wakati upasuaji ukiendelea alihisi kama yuko Senegal na wakati alipoamka na kuzungumza tena madaktari na wauguzi walifurahi kwakuwa wametimiza lengo lao. toa maoni yako

PICHA ZA NYUMBA YA NEY WA MITEGO

Image
kweli mziki unalipa hebu jionee mwenyewe toa maoni yako.........

WizKid na Chris Brown waingia studio

Image
mkali wa "Top your mater" kutoka Nigeria anayefanya vizuli balani Africa pamoja na kupenyeza penyeza katika anga za duniani WIZ KID aingia studio na CRIS BROWN kwa lengo la kufanya ngoma na na mkali huyo kutoka nchini Marekani Kupitia mitandao ya kijamii WizKid ameweka picha hii akiwa na Chris Brown na kuandika “Studio!! @chrisbrownofficial @__bu x Tyga!! #DisturbingLA!” toa maoni yako..........

FABREGAS ATUA CHELSEA KWA PAUNI MILIONI 30

Image
KIUNGO wa Barcelona na Hispania, Cesc Fabregas amejiunga na Klabu ya Chelsea kwa pauni milioni 30 kwa mkataba wa miaka mitano. Fabregas atavaa jezi namba nne kama aliyokuwa akivaa Arsenal na Barcelona.  Kiungo huyo ameishukuru Barcelona ambapo amekaa miaka mitatu kwa furaha. "Ilikuwa timu yangu ya utotoni na nitajivunia kila mara kupata nafasi ya kuchezea timu hiyo kubwa" "Nahisi bado sijamaliza kazi katika Premier League na kwa sasa ni muda muafaka mimi kurudi England… roa maoni yako

Robot yenye uwezo na hisia za binadamu

Image
 Kampuni ya Soft Bank ya nchini Japan imetoa mpya baada ya kutengeneza Robot ambayo ina uwezo ya kuwasiliana na kusoma hisia za mwanadamu. Robot hiyo iliyopewa jina la Pepper inadaiwa kuwa ina uwezo wa kufikiri kama mwanadamu na kufanya kile mtu atakachomwambia na uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali kama binadamu. robot hiyo yenye urefu wa futi nne ni Robot ya kwanza yenye moyo ambapo ina uwezo kutambua sauti, ishara, maneno kupitia programu ya akili bandia iliyofungwa (emotional engine) toa maoni yako.........

MTOTO WA R KELLY ASISAMUA WATU BAADA YA KUTAKA KUBADILI JINSIA

Image
Mtoto wa mwanamuziki mkongwe wa R&B wa nchini Marekani R Kelly ametangaza kubadilisha jinsia yake kupitia mitandao ya kijamii. Mtoto JAYA alizaliwa mwanamke lakini akachukua uamuzi mgumu na kuwaambia mashabiki kuwa sasa hivi yeye ni mwanaume na jina lake ni JAY kwakuwa amebadilisha jinsia yake. Lakini wakati mama yake Andrea Kelly akimuunga mkono mtoto wake kutokana na hatua hiyo, baba yake R Kelly bado hajazungumza chochote na mashabiki wa R Kelly wanasubilia kwa hamu kauli yake kuhusu maamuzi ya mtoto wake.  Jay amesema mama yake alifurahishwa sana kwa kitendo chake hicho na kusema anampenda mtoto wake vyovyote vile alivyo ambapo anamshukuru mama yake kwa kukubali yeye kubadili jinsia yake na kuwa mwanaume.  Pia ameongeza kuwa anaamini yeye sasa ni mwanaume na anataka upasuaji zaidi na tiba ya kumsaidia kuwa vile alivyotakiwa. Jay amesema akiwa na umri wa miaka sita alijigundua kuwa anavutiwa sana na wasichana lakini hataki mahusiano kwanza.