ubaguzi wa rangi bado unaendelea Kenya
Hii ni story ambayo tangu siku ya kwanza iliposikika toka Kenya imeendelea kukaa kwenye headlines kila siku, ishu ya kwanza ilikuwa utaratibu ambao mgahawa huo imeuweka, yani ikifika saa 11 jioni hakuna mtu mweusi alikuwa akiruhusiwa kuingia.. Hofu yao ni Al-Shabaab!
Kingine kilichosikika kuhusu mgahawa huo ni ishu ya lori la mgahawa huo kukutwa katika mtaa wa Kawangware nchini humo likiwa linatupa nyama zilizooza.
Watu watatu akiwemo mchina mmoja waliokamatwa kwenye gari hilo walifikishwa Mahakama ya kaunti ya Nairobi kujibu mashtaka ya kutupa nyama eneo lisiloruhusiwa.
baada ya hayo ni ishu ya
mgahawa huo kufungwa huku wamiliki wakiwa na kesi ya kujibu
kuhusu utaratibu ambao wameuweka kuzuia watu weusi kuhusishwa na ubaguzi
wa rangi pamoja na kugundulika kufanya biashara bila leseni.
Manager wa Mgahawa huo Esther Zao jana amefikishwa Mahakamani na kurudishwa gerezani baada ya Mahakama kuzuia dhamana yake.
Mgahawa huo kwa sasa umefungwa na hakuna
mfanyakazi yoyote anayeruhusiwa kuingia, wafanyakazi wa mgahawa huo
wamesema walitumiwa ujumbe mfupi uliowataka wasirudi kazini hadi
watakapoambiwa wakachukue mshahara wao.
Comments
Post a Comment