Rozi Muhando kumekucha

Sifa za Rose Mhando zaleta utata mtandaoni
Mwanamuziki wa Injili kutoka Tanzania Rose Muhando ameleta utata mtandaoni baada ya kutoa sifa za kuonyesha kumkubali Mwanamuziki wa Bongo Fleva H-Baba kwa kazi yake mpya Show Time,Rose Mhando alitoa sifa hizo baada ya kushuhudia show aliofanya H Baba na wimbo wake mpya wa Show Time.
Rose Mhando alinukuliwa akisema kuwa show aliyoiona kwa H Baba na huo wimbo wake mpya ni matata sana na kama akiendelea kutoa nyimbo kama hiyo hakika wasanii wenzake watashidana sana lakini hawataweza kumfikia,lakini pia aliongeza kuwa H Baba ni msanii ambae anakuwa toka alipoanza kutoka na Mpenzi Bubu amekuwa anazidi kupanda
Baada ya watu kuonyesha hawajapendezwa na kitendo alichokifanya mwanamuziki huyo wa Injili kukubali nyimbo za kidunia, H baba alisema kuwa Rose Mhando ni mwanamuziki mwenzake hivyo haoni kama kuna ubaya yeye kumsifia kwani alichosifia amesifia sanaa yake na si kitu kingine hivyo hakuna tatizo lolote.
"Hebu punguzeni kelele Rose Mhando amenisifia baada yakuona Show yangu wimbo nilioimba ukamvutia ni Show Time na upande wa Show pia jukwanii hilo linafahamika ila linachengeshwa kila siku ila Mungu ananisimamia nipo mpaka leo, Mbona Alli Kiba amesifia show zangu hamjaongea kitu,hii imeingia kwenye historia ya nchi tayari.Ahsante dada angu Rose Mhando nakukubali sanaa." Aliongeza H-Baba.

Comments

Popular posts from this blog

soma habali za kwenye magazeti leo

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z