polisi Marekani yashutumiwa kwa ubaguzi
Ripoti kutoka nchini Marekani zinasema uchunguzi uliofanywa na Wizara ya Sheria kuhusu tukio la mauaji yaliyotekelezwa na Polisi dhidi ya Kijana mweusi mjini Ferguson umebaini kuwepo kwa viashiria vya upendeleo na ubaguzi mjini humo kwenye idara ya Polisi, mahakama na Mfumo wa Magereza.
Akizungumza kabla ya kutolewa kwa Ripoti , Maafisa wamesema Polisi walitumia nguvu kubwa wakabili Watu weusi pia mara kadhaa wamekuwa wakiwashutumu kwa makosa yasiyo na msingi.
Kijana mweusi , Michael Brown, alipigwa risasi na Askari wa kizungu.Maandamano yaliibuka mjini Missouri baada ya mauaji hayo, kisha baada ya jaji kuamua kutomshtaki Afisa wa Polisi
Matokeo ya Uchunguzi uliofanywa na Wizara ya Sheria yanatarajiwa kuchapishwa siku ya jumatano.
Comments
Post a Comment