facebook yapambana na mauaji

Mtandao wa Facebook umeanzisha Nyenzo mpya nchini Marekani kuwasaidia watumiaji wenye mashaka na marafiki ambao wako hatarini kujiua.
Nyenzo hii itawasaidia watu kuripoti ujumbe ambapo ripoti hizo zitaufikia mtandao wa facebook kwa haraka.
Afisa Mkakati wa Mtandao wa Facebook, Holly Hetherington amesema mara nyingi Marafiki na Familia wamekua wakishuhudia hali ya hatari kupitia ujumbe unaowekwa lakini wamekuwa wakishindwa kujua cha kufanya.
Awali watumiaji wa facebook walikuwa wakiandika ujumbe kwenye kurasa zao kuhusu kujitoa uhai lakini hakuna hatua zilizochukuliwa kwa wakati.
Namna gani Nyenzo hii itafanya kazi?

''Mtu atakayeweka ujumbe ataona skrini ikiwa na anuani ambayo itawawezesha kupeleka ujumbe huo kwa Mtu ambaye yuko hatarini kujiua,kuwasiliana na rafiki mwingine kwa ajili ya kuomba msaada au facebook kwa ajili ya kuomba msaada kwa Wataalamu wa kushughulikia ujumbe wenye dalili za hatari ili kupata mwongozo''.Watafiti wa Chuo kikuu cha Washington wameeleza.
Facebook itapitia ujumbe uliowekwa na kama mtu aliyeweka ujumbe hatarishi atabainika kuwa katika hali ya kutia wasiwasi ujumbe wa kumshauri kupata msaada utapelekwa kwake.
Mfano, Serikali ya Wanafunzi ya Forefront imekuwa ikifanya kazi na Facebook, imetengeneza picha za video ambazo zimekuwa zikifundisha namna ya kukabiliana na mawazo ya kujitoa uhai.
Meneja wa Operesheni Paul Miller alikuwa na rafiki ambaye walikuwa wote darasa moja, rafiki yake huyo alijiua miaka mitano iliyopita.
Alibaini hali hiyo baada ya Ujumbe wa Facebook aliouweka kwenye ukurasa wake jioni moja uliosema ''Mambo yamezidi,siwezi kuvumilia tena''.
Miller alimpigia simu rafiki yake huyo siku ya pili asubuhi na kubaini alikwishakufa.
''Sikupata mafunzo, sikujua cha kufanya'' Alieleza Miller.

Comments

Popular posts from this blog

soma habali za kwenye magazeti leo

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z