Posts

Showing posts from March, 2015

angalia video mpya ya diamond platnum ft Khadija kopa taarabu

wimbo mpya kutoka kwa diamond platnum ft Khaduja kopa nasema na wewe bonyeza link hii kuiona video hiyo https://www.youtube.com/watch?v=moE_dXt6-CQ

Kassim Mganga akimbia na hela za studio

Soudy Brown wa Clouds fm ana story hii ya kutokea ugomvi kwenye studio moja Dar kulitokea mtafaruku uliowahusisha wasanii wawili huku chanzo kikidaiwa kuwa ni fedha. Mshiriki wa BBA 2012, ambae ni msanii  wa Bongo Fleva Julio amesema kulikuwa na kuto kuelewana kati ya management yake na ya Kassim Mganga, ambapo walikubaliano kufanya kazi na Kassim lakini wakati wa kukabidhiana kazi  hiyo aligundua studio hiyo imefanya kinyume na makubaliano yao kwa madai kuwa hela aliyotoa hawakuipata. Julio amesema hela ya kulipia studio kwa ajili ya kufanya wimbo huo alimpatia Kassim, lakini studio wanasema hela haikufika. Soudy Brown alimtafuta Kassim lakini hakujibu kitu chochote kuhusu hilo simu ikakatika.

ubaguzi wa rangi bado unaendelea Kenya

Image
Hii ni story ambayo tangu siku ya kwanza iliposikika toka  Kenya imeendelea kukaa kwenye headlines kila siku, ishu ya kwanza ilikuwa utaratibu ambao mgahawa huo imeuweka, yani ikifika saa 11 jioni hakuna mtu mweusi alikuwa akiruhusiwa kuingia.. Hofu yao ni Al-Shabaab! Kingine kilichosikika kuhusu mgahawa huo ni ishu ya lori la mgahawa huo kukutwa katika mtaa wa Kawangware nchini humo likiwa linatupa nyama zilizooza. Watu watatu akiwemo mchina mmoja waliokamatwa kwenye gari hilo walifikishwa Mahakama ya kaunti ya Nairobi kujibu mashtaka ya kutupa nyama eneo lisiloruhusiwa. baada ya hayo ni ishu ya mgahawa huo kufungwa huku wamiliki wakiwa na kesi ya kujibu kuhusu utaratibu ambao wameuweka kuzuia watu weusi kuhusishwa na ubaguzi wa rangi pamoja na kugundulika kufanya biashara bila leseni. Manager wa Mgahawa huo  Esther Zao  jana amefikishwa Mahakamani na kurudishwa gerezani baada ya Mahakama kuzuia dhamana yake. Mgahawa huo kwa sasa umefungwa na hakuna mfa...

soma habali za kwenye magazeti leo

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, imewataja vigogo wanaohodhi maeneo makubwa ya ardhi bila ya kuyaendeleza na kuwapa siku 90 kuhakikisha  wanayaendeleza, kinyume chake yatachukuliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya  Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Tatu Suleiman, ilisema vigogo hao walinunua mashamba katika eneo hilo na kuyaacha muda mrefu bila kuyaendeleza akiwamo mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Mama Ester Sumaye ambaye anamiliki mashamba mawili yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 240 eneo la Misufini, Kibaha vijijini. Taarifa hiyo inawataja watu wengine maarufu ambao wameshindwa kuyaendeleza mashamba hayo kuwa ni,  Phillipo Marmo ambaye ni Balozi wa Tanzania Ujerumani anayemiliki shambamaeneo ya Kikongo, Nicodemus Banduka ambaye ni mkuu wa mkoa mstaafu wa mikoa ya Pwani, Iringa na Mtwara anayemiliki shamba eneo la Vikuge ambalo alilipata mwaka 2000 na  Kipi Warioba aliyewahi kuteuliwa kugombea U...

chanzo cha bifu la Nahreel na Quick Rocka

Kama utakuwa unakumbuka mwaka jana rapper Quick Rocka baada ya kufungua studio yake mpya inayoitwa Switch Records alitangaza kuwa Nahreel ndiye atakuwa mtayarishaji (producer)  wa studio hiyo mpya. Kilichofuatia ni hiki ambacho kimekuwa kinasikika sana, eti ni kweli mastaa hao hawaelewani? Hizo zilizanza wakati ambao Nahreel aliondoka kwenye studio hiyo na kuamua kufungua ya kwake iitwayo The Industry. Akizungumza na millardayo.com producer Nahreel alifunguka na kusema; “Kiukweli is true sielewani na Quick Rocka na kwa sababu yeye anadai kuwa mimi niliondoka studio kwake kiswahili bila kumtaarifu.. huenda ni kweli niliondoka hivyo lakini Quick Rocka mimi  hakuniajiri kama mwajiriwa wake Switch Records.. sisi tulikuwa tunafanya kazi kiushikaji na mimi nilikuwa na mipango yangu ya kufungua studio lakini pengine labda jamaa hakupenda kile kitendo cha mimi kuondoka pale“– Nahreel. “Natafuta jinsi ya kukaa naye na kuongea kama binadamu ili tuyaweka haya mambo sawa, nimekosa huo ...