Jack Patrick apewa hukumu ndogo China
BAADA ya kushikiliwa kwa takriban miezi tisa kwa kesi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye Video Queen maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela huku kukiwa na uwezekano wa kupunguziwa adhabu ikawa ndogo zaidi, Amani linaibumburua habari kamili. HUKUMU NYEPESI? Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Jack, modo huyo alihukumiwa Jumatatu iliyopita (Agosti 11, mwaka huu) kwenye Mahakama ya Macau huko Hong Kong ambapo hukumu hiyo ilitofautiana na adhabu nyingine za madawa nchini humo ambazo huwa hukumu yake ni kunyongwa hivyo ya Jack kuonekana nyepesiii! KWA NINI NYEPESI? Kikimwaga data, chanzo hicho makini kilidai kwamba, hukumu hiyo ya Jack ni nyepesi ukilinganisha na hukumu nyingine za madawa ya kulevya zinazotolewa nchini China ambapo hakimu alitumia muda wa dakika 27 tu kuisoma. “Hukumu za madawa ya kulevya zinatofautiana nchini China. Kuna baadhi ya majimbo kama Beijing huwa wao ikithibitika umebeba madawa ya kulevya, una...