Vanessa Mdehe aichukua nafasi ya Diamond Kwenye show Marekani
Vanessa Mdee ataungana na wasanii ‘cream’ kutoka Afrika kwenye tamasha la mara ya pili la One Africa Music litakalofanyika jijini Houston, Texas, Marekani, October 22.
Hiyo itakuwa show ya pili baada ya ile ya kwanza iliyofanyika July 22, kwenye ukumbi wa Barclays Centre, New York, Marekani na kukutanisha mastaa kama Diamond, Wizkid, Davido, Tiwa Savage, Flavour na wengine.
Katika show ya October 22, Vanessa Mdee apanda jukwaa moja na wasanii wakubwa wa Afrika wakiwemo 2 Face, Flavour, P –Square, D’Banj, Kcee, Mafikizolo, Fally Ipupa na Cabo Snoop,
“Houston we have a PROBLEM!!!!! See you at the Toyota Centre on the 22nd Oct 2016,” ameandika Vee Money.
“Watu wangu wa Houston na miji mingine ya karibu. Nataka kuwaona kwa wingi.”
Comments
Post a Comment