CCM YAZUIA UKAWA KURUSHA MATANGAZO KATIKA TELEVISHENI?

Vyama vya Chadema na CCM vimeingia katika mchuano wa kuwania nafasi ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya kampeni za wagombea urais katika televisheni Jumamosi hii.
Wakati Chadema ikitaka muda wa kurusha matangazo ya uzinduzi wa kampeni za mgombea wake, Edward Lowassa kutokea jijini Dar es Salaam, CCM inataka kurusha matangazo ya mkutano wa kampeni ya mgombea wake, Dk John Magufuli kutoka jijini Mbeya.
Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema jana kuwa kumekuwa na njama za CCM kutaka kuzuia fursa ya Chadema kurusha kampeni za mgombea wake kwa kutaka siku hiyo irushe kampeni za Dk Magufuli.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikiri chama hicho kutaka kurusha matangazo ya mgombea wake na kuhoji; “tatizo liko wapi kama Chadema imechelewa kulipia?”
“Ni kweli mgombea wetu wa urais akiwa Mbeya tutarusha matangazo ya kampeni zake moja kwa moja kwenye runinga, sasa ni runinga ngapi siwezi kujua maana kuna watu wanalifanyika kazi suala hilo. Lakini kama Chadema walijua wana tukio lao kwa nini wasingewahi kulipia?” alihoji.
Chanzo cha habari kutoka kituo kimoja maarufu, kimeeleza kuwa kwa nyakati tofauti, CCM na Chadema waliomba muda wa kurusha vipindi vyao, lakini CCM ndiyo waliofanikiwa kupata.
“Ninachojua hao wote walikuja kwa nyakati tofauti kuomba muda na CCM ndiyo waliofanikiwa kupata,” alidokeza mmoja wa wafanyakazi wa telesheni hiyo ambaye hakutaka kutaja jina kwa maelezo kuwa siyo msemaji.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Azam TV, Tido Mhando alisema CCM na Chadema vilikuwa vimeomba kurushiwa matangazo yao na vyote vimelipia. Alisema kila moja kitapata fursa hiyo kwa kuwa kituo chake kina channel nyingi mgombea wake, Dk John Magufuli kutoka jijini Mbeya. Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema jana kuwa kumekuwa na njama za CCM kutaka kuzuia fursa ya Chadema kurusha kampeni za mgombea wake kwa kutaka siku hiyo irushe kampeni za Dk Magufuli.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikiri chama hicho kutaka kurusha matangazo ya mgombea wake na kuhoji; “tatizo liko wapi kama Chadema imechelewa kulipia?”
“Ni kweli mgombea wetu wa urais akiwa Mbeya tutarusha matangazo ya kampeni zake moja kwa moja kwenye runinga, sasa ni runinga ngapi siwezi kujua maana kuna watu wanalifanyika kazi suala hilo. Lakini kama Chadema walijua wana tukio lao kwa nini wasingewahi kulipia?” alihoji.
Chanzo cha habari kutoka kituo kimoja maarufu, kimeeleza kuwa kwa nyakati tofauti, CCM na Chadema waliomba muda wa kurusha vipindi vyao, lakini CCM ndiyo waliofanikiwa kupata.
“Ninachojua hao wote walikuja kwa nyakati tofauti kuomba muda na CCM ndiyo waliofanikiwa kupata,” alidokeza mmoja wa wafanyakazi wa telesheni hiyo ambaye hakutaka kutaja jina kwa maelezo kuwa siyo msemaji.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Azam TV, Tido Mhando alisema CCM na Chadema vilikuwa vimeomba kurushiwa matangazo yao na vyote vimelipia. Alisema kila moja kitapata fursa hiyo kwa kuwa kituo chake kina channel nyingi

Comments

Popular posts from this blog

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z

mbinu za kuwa producer au mtayarishaji wa music