wadau wa muziki waijia juu BASATA baada ya kumsimamisha Shilole kufanya muziki mwaka mmoja
kumekuwa na na mawazo tofauti ya wadau mbalimbali kuhusiana na taarifa iliyotolewa na basata ya kumsimamisha mwanadada Shilole kufanya muziki kwa muda wa mwaka mmoja
na haya ni baadhi ya malalamiko ya wadau wa muziki kupitia mitandao ya kijamii
Sain Meles HABARI
HII SIYO NZURI , HII INARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WASANI HUSUSAN
WAKIKE WANAOFANYA VIZURI NCHINI AMBAO NAO BADO NI WACHACHE , Hata hivyo
Shilole hakucheza uchi kama inavyo daiwa , ziwa lake lilitoka nje kwa
bahati mbaya akiwa stejini pia aliwai
kuwaomba Watanzania msamaha kwa kile kilichotokea, ingawaje BASATA
mnalikuza tukio hilo kama vile bado analiendeleza, Kwahiyo mnamsitisha
kufanya Music mnataka afanye nini? Vipi familia ndugu na jamaa zake
wanaonufaika kupitia kazi zake? Adhabu ya Mwaka mmoja ni kumrudisha
nyuma kimaendeleo , Hivi mnajua Shilole ameteseka kiasi gani mpaka kuwa
Star Hapa bongo? Nadhani hamlifahamu hilo ndiyo maana mnachukulia poa.
Nawe Mtanzania unaeshangilia Kufungiwa kwake inakusaidia nini , Wewe ni
Msafi , mkamilifu na wala hukosei katika jamii inayo kuzunguka ? BASATA
mgefanya mpango hata video za Nje zisifike Tz , Maana mnakwepa mkojo tu
ila M*** bado mnayakanyaga...
Ezekiel Kessy BASATA
hawajatumia busara kwa maana huyo ni mwanake na mkimfungia mziki
mnategemea atapata wapi kipato cha kumkimu kimaisha ni bora mmwambie
alipe faini na aendelee na mziki na siyo kumfungia
Ibrah Mussa Maganga BASATA
ni wapuuzi tuu kwanini wamfungie shilole wakati kuna TELEVISHEN
zinaonesha video za utupu za wasanii wa nje kwani wenyewe hawapotoshi
maadili ya watanzania?Hi dunia sahv kila mtu anafanya anachopenda kwenye
roho zao wangapi BONGO MOVIE wanacheza movie waki uchi?mfano filamu YA
OPRAH ilikuwa na maadili gani? huo ni uonevu dunia hii ni huru bhana!
imeandaliwa na team miki
Comments
Post a Comment