ataka ubunge kisa kasoma na Magufuli

Baada ya Urais sasa Vituko vimeanza katika kampeni za kuwania kuteuliwa na CCM kugombea nafasi za Ubunge katika majimbo mbalimbali nchini.

Moja ya vituko hivyo ni kile kilichotolewa na Mbunge wa Dodoma Mjini anayemaliza muda wake Dk.David Mallole ambaye jana wakati akijinadi kwa wanachamawa chama hicho, aliwaomba wamteuwe kwa mara nyingine kwa sababu amesoma darasa moja na mgombea Urais John Magufuli.

Wakati hayo yakijiri Dodoma, Jimbo la Kinondoni msanii Steve Nyerere aliomba achaguliwe kwani ana uwezo wa kupita katika ofisi za mabalozi wa nje waliopo jijini Dar es salaam kuomba misaada.

Kampeni hizo zilianza jana wakati Dar wakati wagombea wakijinadi mbele ya wajumbe kabla ya kupiga kura ya maoni Agosti mosi mwaka huu.

“Wilaya ya Kinondoni ndio inayoongoza kwa kuwa na ofisi nyingi za mabalozi, mkinichagua nitahakikisha nakwenda wenye Ubalozi wa Marekani kuomba misaada kwa ajili ya kuwawezesha vijana…Nitakwenda Ubalozi wa China kuomba atusaidie kuondoa mafuriko yanayolijumba jimbo hili “Steve Nyerere.

Katibu wa CCM,Kinindoni alisema katika Wilaya yake kuna wagombea 60 ambao kati yao wanawake wanne wanawania majimbo ya Kinondoni,Kawe, Ubungo na Kibamba.

Comments

Popular posts from this blog

soma habali za kwenye magazeti leo

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z