Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, imewataja vigogo wanaohodhi maeneo makubwa ya ardhi bila ya kuyaendeleza na kuwapa siku 90 kuhakikisha wanayaendeleza, kinyume chake yatachukuliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Tatu Suleiman, ilisema vigogo hao walinunua mashamba katika eneo hilo na kuyaacha muda mrefu bila kuyaendeleza akiwamo mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Mama Ester Sumaye ambaye anamiliki mashamba mawili yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 240 eneo la Misufini, Kibaha vijijini. Taarifa hiyo inawataja watu wengine maarufu ambao wameshindwa kuyaendeleza mashamba hayo kuwa ni, Phillipo Marmo ambaye ni Balozi wa Tanzania Ujerumani anayemiliki shambamaeneo ya Kikongo, Nicodemus Banduka ambaye ni mkuu wa mkoa mstaafu wa mikoa ya Pwani, Iringa na Mtwara anayemiliki shamba eneo la Vikuge ambalo alilipata mwaka 2000 na Kipi Warioba aliyewahi kuteuliwa kugombea U...
Comments
Post a Comment