chuo kikuu Kenya chavamiwa
Stori ambayo imechukua Headlines tangu asubuhi ya
leo April 02 ni taarifa kutoka kwa wenzetu Kenya kutokana na lile
shambulio la kigaidi limehusishwa na kikundi cha Kigaidi cha Al-Shabaab
na hii ni baada ya kuvamia Garissa College University, huu ni muendelezo wa kile kilichoripotiwa mwanzo.
Mpaka sasa ripoti inasema Wanafunzi 70, wameuawa
na wengine zaidi ya 79, wamejeruhiwa kutokana na tukio la uvamizi wa
Garissa College University, wanafunzi walionusurika wamesema magaidi hao
walianza kuwapiga risasi walinzi wawili waliokuwa getini na kuelekea katika
mabweni ya wanafunzi ambapo walianza kuwagawa kwa dini zao na kuanza kuwaua kwa
risasi.
Kufuatia tukio hilo Rais
Uhuru Kenyatta, amemtaka Inspector Generali wa Polisi, Joseph Boinet kuhakikisha wanamgambo wote wanaripoti
kwenye chuo cha mafunzo ili kuongeza idadi ya maafisa wa Polisi nchini humo.
Amesema taifa hilo linakubwa na uhaba wa maafisa
wa Polisi kutokaza na kufutwa kwa zoezi la kuwasajili maafisa wa Polisi, Serikali
ya Kenya imetangaza kumzawadia shilingi milioni ishirini za Kenya mtu yoyote
atakaefanikisha kukamatwa kwa mshukiwa mkuu wa shambulio hilo anaefahamika kama
Mohhamed Mahamoud, Polisi
bado wanaendelea na zoezi la uokoaji.
chanzo millardayo.com
Comments
Post a Comment