Ukawa wamtia kitanzi Sitta
UAMUZI uliofikiwa na viongozi wa vyama vya siasa na Rais Jakaya Kikwete umemweka katika wakati mgumu Mwenyeki wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta kuahirisha au la vikao vya Bunge hilo. Hii inafuatia Rais Kikwete na viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kukubaliana kusitisha Bunge la Katiba Oktoba 4 tofauti na ratiba ya Sitta ambayo inaonyesha vikao vitaendelea hadi Oktoba 31 atakapomkabidhi rais katiba iliyopendekezwa. Vilevile kwa tafsiri ya uamuzi huo, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) watakuwa wameibuka kidedea kwani tangu mwanzo walikuwa wanataka Bunge hilo liahirishwe hadi maridhiano yapatikane. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo, alisema katika makubaliano ya kikao chao na rais kilichofanyika juzi Ikulu ndogo mjini hapa, walikubaliana kwa pamoja kuwa Bunge la Katiba liendelee hadi Oktoba 4. Kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa imetolewa mara baada ya awamu ya pili ya Bunge la Katiba kuanza Oktoba 10 hadi 21, ndiyo waju...