joh makin kufanya collabo na msanii wa nigeria

Coke Studio ni project inayokutanisha wasanii mbalimbali wa Afrika ambao mbali na kupata nafasi ya kufahamiana lakini pia inawapa fursa ya kuweza kushirikiana kwa kufanya nyimbo pamoja na kutengeneza network mpya katika nchi wanazotoka.

Mwamba wa Kaskazini mwaka huu ni miongoni mwa wasanii waliopata shavu hilo, na kwa sasa yupo jijini Nairobi alikosindikizwa na G-Nako. Akiwa kwenye project hiyo Joh amefanikiwa kufanya collabo na muimbaji wa kike kutoka Nigeria, Chidinma katika studio ya RKay na kufanya uhusiano kati ya wasanii wa Tanzania na Nigeria uzidi kukua.

Kupitia Instagram Joh Makini ameandika:
“Shukurani sana kwa producer @rkaykamanzi @gnakowarawara na mwanadada @chidinmaekile leo nimemuimbisha kiswahili asante @cokestudioafrica kwa kutuleta pamoja #cokestudioafrica

Comments

Popular posts from this blog

soma habali za kwenye magazeti leo

hii ni list ya baadhi ya majina ya wasanii wa Nigeria waliohit mwaka huu kuanzia A-Z