Posts

Showing posts from July, 2014

mbinu za kuwa producer au mtayarishaji wa music

imeandikwa na prod. MicMarryEd micmarryed@gmail.com tzmusic21@gmail.com 0716842016 0755776236 Producer/ ntayarishaji wa music wa audio ni mtu anayetengeneza nyimbo zilizo katika mfumo wa audio. kuna siri nyingi za kuweza kuwa producer lakini kwa leo naomba tuanze na hizi. 1. nia - kwa kawaida ukitaka kufanya kitu chochote na kufanikiwa lazima uwe na nia ya kufanya kitu hicho hapo utafanikiwa 2. maamuzi - ukishakuwa na nia lazima ufanye maamuzi ya moja kwa moja ambayo unayapa marks 100 ambayo hayatakughalimu 3. kujitoa - ukishafanya maamuzi nilazima ukubali kujitoa kwa maana kazi ya production ni lazima kujitoa na usipojitoa kwa moyo wote hauwezi kufanya kazi nzuri 4. kujituma - mafanikio yooote yanakuja kwa kujituma usipojituma hauewezi kupata chochote utaishia tu kuwasifia watu kuwa mtu flrni mkali sana yani anapiga beati kali balaa 5. kuwa na moyo - ukishajituma nilazima uwe na moyo wa kujifunza na kuto kukata tamaa kwa sababu watu wengi huwa wanakuwa wanawahi kukat...

ndege nyingine ya Malaysia iliyoanguka Ukraine

Image
Ndege ya Malaysia iliyokuwa imebeba abiria 295 ndani yake imeanguka Mashariki mwa Ukraine ikitokea Amsterdam kwenda Kuala Lumpur, kufuatia tuhuma kuwa ilitunguliwa. Miili kadhaa ya watu imesambaa katika eneo ilipoanguka ndege hiyo karibu na kijiji cha Grabovo, kinachodaiwa kushikiliwa na waasi. Ndege hiyo ya MH17 ilikuwa inakaribia kuingia katika ardhi ya Urusi wakati ilipopoteza mawasiliano. Pande zote mbili serikali ya Ukraine na waasi wamekanusha kuitungua ndege hiyo katika mji ulio karibu na mpaka wa Urusi. chanzo cha habali.... millardayo.com toa maoni yako.............

wema na penny bifu basi tena

Image
STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amesema baada ya kutokuwa na maelewano kwa muda mrefu na mtangazaji maarufu Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’, sasa ameamua kumsamehe rasmi kwa heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Staa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Wema alisema: “Kwa moyo mweupe, nasema nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye popote nitasalimiana naye kama kawaida. Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti wa Kiislam na nahitaji sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa Mungu.” Mtangazaji maarufu Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’. Kwa upande wa Penny alifunguka: “Siwezi kusema nitamchukia Wema ila nimekubali matokeo, sina tatizo naye tena ingawa najua hatuwezi kuwa marafiki tena  kama zamani, lakini yaliyopita yameshapita.” Wema na Penny walikuwa na bifu kwa muda mrefu, chanzo kikiwa Penny kuingilia uhusiano wa Wema kwa Mwanabongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.     

joh makin kufanya collabo na msanii wa nigeria

Image
Coke Studio ni project inayokutanisha wasanii mbalimbali wa Afrika ambao mbali na kupata nafasi ya kufahamiana lakini pia inawapa fursa ya kuweza kushirikiana kwa kufanya nyimbo pamoja na kutengeneza network mpya katika nchi wanazotoka. Mwamba wa Kaskazini mwaka huu ni miongoni mwa wasanii waliopata shavu hilo, na kwa sasa yupo jijini Nairobi alikosindikizwa na G-Nako. Akiwa kwenye project hiyo Joh amefanikiwa kufanya collabo na muimbaji wa kike kutoka Nigeria, Chidinma katika studio ya RKay na kufanya uhusiano kati ya wasanii wa Tanzania na Nigeria uzidi kukua. Kupitia Instagram Joh Makini ameandika: “Shukurani sana kwa producer @rkaykamanzi @gnakowarawara na mwanadada @chidinmaekile leo nimemuimbisha kiswahili asante @cokestudioafrica kwa kutuleta pamoja #cokestudioafrica

irene uwoya afanya fujo kwa mume wa mtu

NYOTA wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amesababisha tena! Safari hii amekinukisha nyumbani kwa mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi wake (jina tunalo) kufuatia jamaa huyo kufunga ndoa na mwanamke mwingine na kumfanya Uwoya kuendelea kuwa ‘nyumba ndogo’. Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilichukua nafasi juzikati, nyumbani kwa mwanaume huyo, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam. MCHEZO ULIVYOKUWA Chanzo kilidai kwamba, siku ya tukio, Uwoya akiwa na baadhi ya mastaa wenzake (hawakutajwa) kwenye kambi ya maandalizi ya kurekodi filamu mjini Bagamoyo, Pwani, alipokea simu iliyomnyetishia kuwa, mpenzi wake huyo amefunga ndoa na mwanamke mwingine jijini Mwanza, kwa hiyo yeye aliye tu! UWOYA ACHANGANYIKIWA “Uwoya alipopata salamu hizo kwa njia ya simu alichanganyikiwa! Alianza kusema maneno ya kumshutumu waziwazi huku akiangua kilio. Mbaya zaidi aliyemjulisha ishu hiyo alisema ndoa hiyo ilishafungwa na si kwamba ipo kwenye maandalizi. “Akasema anaondoka kambini kumfuata ...

matokeo ya kidato cha sita 2014

hii ndio link ya matokeo ya kidato cha sita 2014 http://www.necta.go.tz/matokeo2014/ACSEE.htm

msanii wa kizazi kipya gumzo ujelumani

Image
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Malfred Alfred ameweza kukonga nyoyo za mashabiki katika tamasha kubwa la muziki liliobatizwa jina Jugend-festival Iller-tissen 2014 lililofanyika hivi karibuni nchini Ujerumani. 0 Msanii wa bongo Malfred Alfred Malfred ameiambia eNewz kuwa hii imekuwa ni nafasi kubwa kwake kwa kupata mwaliko huo akiwa kama mgeni kutoka barani Afrika ambapo ameweza kupaform jukwaa moja na bendi maarufu za nchini humo zikiwemo 'like the Killerpilze' na 'Qunstwerk!! Aidha Malfred ameelezea kuwa hivi sasa anaendelea kuutangaza muziki wake nchini Ujerumani huku akiwa amefanya kolabo mpya na msanii Kala Jeremiah katika wimbo wao mpya uliobatizwa jina 'Usipoteze Time. Tags:  msanii wa muziki Tanzania Malfred Alfred

nchi ya Brunei yapitisha sheria ya wezi kukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe

Image
  Sultani na mtawala wa Brunei ambaye ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani Serikali ya Brunei iliyo Kusini Mashariki mwa Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za kiisilamu. Kiongozi wa nchi hiyo ya kiisilamu ambayo ni jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia wiki hii. Adhabu zilizo chini ya sheria za kiisilamu ni pamoja na kuwakata wezi mikono na kuwapiga mawe hadi kufa watu waliopatikana na hatia ya kushiriki Zinaa. Sheria hii itatekelzwa katika awamu tatu katika kipindi cha miaka mitatu. Umoja wa Mataifa tayari umeelezea wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo. Taifa la Brunei tayari linafuata sheria kali za kiisilamu kuliko hata nchi jirani kama Malaysia na Indonesia pamoja na kuharamisha uuzaji na utumiaji wa pombe. Nchi hiyo ndogo ilio katika kisiwa cha Borneo,inatawaliwa na Sultan Hassanal Bolkiah na imepata utajiri wake kutokana na kuuza nje mafuta na gesi yake. Takriban nusu ya waisilamu wanaoishi katika nchi hiyo ni raia wa Malays...

bint anaswa na nguo za kuambiana

Image
AMA kweli duniani kuna sarakasi! Takribani siku kumi tangu alipofariki dunia aliyekuwa ‘kichwa’ kwenye filamu za Kibongo, Adam Phillip Kuambiana (38), mrembo aliyejitambulisha kwa jina Mary Njombe amenaswa na nguo za staa huyo wakati mali za marehemu hazijagawanywa. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu makini, Mary ambaye ni mkazi wa Magomeni Hospitali, Dar amekuwa akipigilia pamba za marehemu hasa baada ya jamaa huyo kutangulia mbele ya haki. “Jamani njooni huku Magomeni Hospitali hapa mtaa wa pili kuna mwanamke anatinga nguo za marehemu Kuambiana,” kilisema chanzo chetu. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walifanya msako eneo hilo hadi wakamnasa Mary. Katika mahojiano na gazeti hili, Mary alisema kuwa alikuwa mchumba wa Kuambiana na alichobahatika kubaki nacho ni nguo ambazo alimpatia mara ya mwisho amfulie (zinaonekana pichani). Mary alisema kuwa yeye na Kuambiana walifahamiana tangu mwaka 2006 ambapo alikuwa akimbembeleza kuwa naye. “Mwaka 2008 ndiyo tulian...

picha ya mzee ambaye hajaoga kwa miaka 37

Image

raisi Kikwete aandaa futari mbeya Jumapili Julai 13, 2014

Image
Mbunge wa Mbeya Mhe Joseph Mbilinyi "Sugu" akipata futari na wananchi wenzie wa Mbeya katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014. Meza Kuu katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014.… Mbunge wa Mbeya Mhe Joseph Mbilinyi "Sugu" akipata futari na wananchi wenzie wa Mbeya katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014. Meza Kuu katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishurkuru wananchi wa Mbeya kwa kujitokeza kwa wingi katika futari aliyoiandaa katika katika u...

mwarabu amliza wema

Image
STAA wa sinema za  Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘ameingizwa mjini’ na mhariri wa filamu Bongo mwenye asili ya Kiarabu aliyejulikana kwa jina moja la Chidy kwa kuingia mitini na shilingi 5,000,000 alizompa ili azihariri filamu zake mbili lakini kazi haikufanyika. Staa wa sinema za  Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu. Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania Kituo Kikuu jijini Dar es Salaam, kilisema ilikuwa mwaka jana (2013) ambapo Wema alimkabidhi mhariri huyo filamu mbili, Super Star na Vian Unaspect. MALIPO YAFANYWA, KAZI HAKUNA Ikazidi kudaiwa kwamba mbali na filamu hizo, Wema alimlipa jamaa shilingi 2,500,000 ili kuzihariri (editing) filamu hizo ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kuingia sokoni. JAMAA AINGIA MITINI, AMKWEPA WEMA Habari zikazidi kudai kwamba, baada ya kuudaka ‘mpunga’ huo jamaa huyo amekuwa akimzungusha Wema kufanya kazi zake na kumkabidhi ili azipeleke sokoni ndipo wiki iliyopita mlimb...

picha za video ya linah aliyoifanya south africa

Image
kwa sasa Linah ni levo za kimataifa amefanya video yake ya kwanza na director wa South Africa Godfather ya wimbo wake mpya uitwao Ole Themba ambayo audio yake amerecord kwenye studio ya Oskido. kwa upande wa video Director Godfather ndiye aliyetengeneza video ya Mdogomdogo ya Diamond,Kerewa ya Sheta na video nyingine za P Square na Davido

tid amtukana ray c matusi ya nguoni

Image
  June 30 kupitia mtandao wa kijamii wa instagram kwenye akaunti ya Tid alipost picha iliyokuwa na maneno >>’Listen to this mix….once again from @lamarfishclub’ ni wimbo ambao ameurudia kwa mtindo anaoufanya Lamar kwa sasa zile Refix. Baada ya kuweka picha hiyo mmoja wa watu waliotoa maoni yao au comments kwa picha hiyo ni mwanamuziki Ray C ambaye aliandika maneno haya yaliyooneka kumkera TID Ray C ameandika “Come let’s talk Tid u are the best musician in East Africa please lets talk” maneno haya hakuna aliyejua Ray C anachomaanisha lakini cha kushangaza na ambacho kimeibua maswali ni jinsi TID alivyojibu comment hiyo. Leo kupitia kipindi cha Xxl Tid ameelezea sababu ya kuandika hivyo ambapo amenukuliwa akisema “Mimi kama kuna mtu ananitafuta hawezi kunitafuta kwenye instagram, sijawahi kuwa na matatizo na Ray C sijamuona nina kama miaka 5 hivi” “Hivi Ray C anataka kukutana na mimi nini anataka kuongea na mimi mbona hajanitafuta miaka yote ananitafuta s...